Mtikisiko wa tano

Dodoma. Bunge jana lilikabidhi ripoti ya uchunguzi wa IPTL kwa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ili ipitie na kutoa mapendekezo bungeni, hatua ambayo inatazamiwa kusababisha mtikisiko wa tano katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika vitabu vitano, ilikabidhiwa na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe huku akimpa masharti ya kuipitia kwa siri, kinyume na Zitto alivyokuwa ameahidi kuwahoji watuhumiwa katika kikao cha wazi.
Ripoti hiyo inatokana na uchunguzi maalumu wa fedha zilizochotwa katika akaunti ya escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), iliyokuwa inatunza fedha za gharama za uwekezaji (capacity charge) kwa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL baada ya kutokea mgogoro wa kibiashara baina yake na Tanesco.
Tanesco ililalamika kuwa ilikuwa inailipa zaidi IPTL kinyume na gharama za uwekezaji hivyo kuamuliwa na Mahakama kuwa fedha ilizokuwa inatakiwa kulipa ziwekwe katika escrow hadi upatikane ufumbuzi wa mgogoro huo.
Hata hivyo, kesi hiyo ilipohukumiwa Februari mwaka huu, ikibainisha kweli Tanesco ilikuwa inailipa zaidi IPTL, ilibainika kuwa fedha zilizokuwa katika akaunti hiyo Sh 306 milioni zilikwishachotwa na IPTL kwa ruksa ya baadhi ya viongozi wa Serikali.
Kutokana na hali hiyo, ripoti hiyo inaweza kuondoka na vigogo waliohusika na kashfa hiyo, kama ilivyowahi kutokea katika kashfa nyingine nne zilizoitikisa Serikali ya Awamu ya Nne ya inayoongozwa na Rais Kikwete
Richmond
Kashfa kubwa iliyotikisa nchi katika kipindi cha awali cha Rais Kikwete ilikuwa ni Richmond ya mwaka 2006. Hii ilitokana na tatizo kubwa la uhaba wa umeme na Serikali kulazimika kutafuta njia za dharura za kutatua tatizo hilo, zikiwamo zilizodaiwa kukiuka taratibu na sheria.
Baada ya kashfa hiyo kuchunguzwa na taarifa kutolewa bungeni, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa alilazimika kujiuzulu baada ya kutakiwa ajipime kutokana na mazingira ya kashfa hiyo.
Wengine waliong’oka madarakani ni mawaziri wa Nishati na Madini kwa vipindi tofauti, Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha.
- Soma Zaidi Hapa(Mwananchi)

Post a Comment

أحدث أقدم