
Anthony Banbury akiwa kwenye kikao maalum na Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf kwenye Ikulu ya nchini hiyo.
Na Mwandishi wetu
Afisa
wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mapambano dhidi ya maradhi ya Ebola
ameionya jumuiya ya kimataifa isilegeze kamba katika harakati za
kuyatokomeza maradhi hayo hatari
Akizungumza
baada ya kukutana na rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf mjni
Monrovia Afisa huyo Anthony Banbury amesema ingawa zipo dalili za
kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo kila mtu anapaswa kuendelea kuwa
makini
Banburry
amesema umoja wa mataifa umejenga vituo vya kupambana na Ebola huku
watu wa kujitolea wakiitajika kuviendesha vituo hivyo.
Wakati huo huo, shirika la afya ulimwenguni WHO limesema majaribio ya chanjo dhidi ya Ebola yameonyesha matumaini ya mafanikio.
إرسال تعليق