
Al Shabaab lakiri kutekelza shambulizi nchini kenya
Kundi la Al Shabaab nchini Somali linasema kuwa limefanya mashambulizi
ya abiria 28 katika basi moja kazkazini mashariki mwa kenya.
Basi hilo ambalo lilikuwa likiwabeba abiria 60 lilitekwa katika jimbo la mandera lilipokuwa likelekea mjini Nairobi.
Abiria
mmoja ambaye alinusurika ameiambia BBC vile raia wasio wa Somali
walitengwa na wengine na wale ambao hawakuweza kusoma aya ya Quran
walipigwa risasi kwa karibu.
Katika taarifa yake al Shabaab
limesema kuwa mashambulizi hayo ni ya kulipiza kisasi mauaji ya waislamu
huko Mombasa yaliotekelezwa na vikosi vya usalama vya kenya.
Kenya
imekumbwa na misururu ya mashambulizi ya risasi na mabomu yanayodaiwa
kutekelezwa na kundi la Alshabaa tangu vikosi vyake viingie nchini
Somali.
- BBC
إرسال تعليق