
Waziri
wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameyashutumu
mataifa ya magharibi kwamba yanataka kubadilisha serikali ya Urusi kwa
kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi, kwa sababu ya mzozo wa Ukraine.
Aliuambia
mkutano wa wataalamu wa mashauri ya nchi za nje mjini Moscow kwamba
mataifa ya magharibi siyo yanataka kuifanya Urusi ibadilishe sera zake
kuhusu Ukraine tu, bali yanataka kubadilisha serikali ya Urusi.Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea Urusi vikwazo kadha vya kiuchumi kwa sababu zinaishutumu kuwa inawasaidia wapiganaji wa mashariki mwa Ukraine.
Bwana Lavrov alisema vikwazo hivyo vililenga kuharibu uchumi wa Urusi na kuchochea maandamano.
- BBC
إرسال تعليق