Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja
kuwa ni miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea
mabilioni kutoka katika akaunti ya escrow.
Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi
wengine wa dini walioingiziwa fedha katika Benki ya Mkombozi
inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa
(Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh40.4 milioni).
Akizungumza kwa simu jana, Askofu Kilaini alisema
Rugemalira hupendelea kuchangia kwa uwazi miradi ya kijamii na si yeye
peke yake aliyempatia mchango, bali kuna watu wengine wengi ambao
wameshampatia na kazi yake ni kuipokea na kuifikisha sehemu husika.
Hata hivyo, kabla hajafafanua zaidi hoja yake, simu ilikatika na baadaye hakupatikana tena.
Hata hivyo, jana askofu huyo alinukuliwa na Gazeti
la Mawio toleo la jana akisema fedha alizozipokea kutoka kwa Rugemalira
ni kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoendeshwa na Kanisa Katoliki.
“Ndiyo nimepokea fedha kutoka kwa James na hii
siyo mara ya kwanza, kwani mara nyingi amekuwa akichangia miradi
mbalimbali ya kijamii,” alisema Askofu Kilaini.
Alipotakiwa na gazeti hilo kuwataja wengine
waliochangia kanisa lake na kama nao wamechanga kutoka kwenye fedha za
akaunti ya escrow, alisema yeye hayumo kwenye michango hiyo.
Alipoulizwa anawezaje kusema hayumo kwenye orodha
ya waliopewa fedha kutoka akaunti ya escrow wakati anakiri kuwa
aliingiziwa mamilioni ya shilingi na Rugemalira, alisema michango
inayoletwa kwake haina siri, hivyo wezi halisi ndiyo wakamatwe.
“Michango inayoletwa kwangu haina siri, shikeni wezi halisi,” alisema.
Askofu Nzigirwa
Kwa upande wake, Askofu Nzigirwa ambaye alirithi
kiti cha Kilaini, cha Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam
ameeleza kushtushwa kwake na ripoti ya PAC iliyomtaja yeye na Kilaini
kuhusika katika uchotwaji wa Sh306 bilioni za escrow.
- Mwananchi
- Mwananchi
Post a Comment