Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
Wakiongea na NIPASHE kwa nyakati tofauti wakazi wa Boko Basihaya, walisema kuwa vurugu zilizuka katika ofisi ya serikali za mitaa baada ya mawakala wa vyama kuingilia kati zoezi hilo kwa kudai kuwa uandikishaji huo haukufuata utatatibu wa mipaka yao na zilitulizwa na polisi waliokuwa wakiangalia usalama katika vituo vya uandikishaki ambao walisimamisha zoezi hilo hadi muafaka upatikane.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju, Emmanuel Riwa, alisema kuwa vurugu hizo zilichukua saa tatu hali iliyochangia kusimamishwa kwa zoezi ili kukaa na mawakala wavyama vyote na kufikia muafaka kuwa sehemu ambayo ina matatizo ya mipaka watajiandikisha wakati mwingine.
Alifafanua kuwa mipaka hiyo ilicheleweshwa na Manspaa ya Kinondoni, baada yakuwapigia simu wameahidi kuwaonyesha mwisho wa wakazi wa Basihaya na mwanzo wa wakazi wa Wazo eneo la kiwanda cha Saruji.
“Uandikishaji unakwenda vizuri ingawa katika kata hii ya Bunju kuna sehemu shida imetokea kutokana na madai ya mipaka ambayo viongozi wa vyama waliwakataza wananchi wao wasiende kujiandikisha kwa madai kuwa sio wakazi wa eneo hilo, kati ya mitaa 41,ni mtaa mmoja tu wa Wazo ndio wenye matatizo, tumesimamisha kwa mda,” alisema.
Hali ya uandikishaji wa wapiga kura katika Jiji la Dar es Salaam umedorora kutokana na viongozi nawatendaji wa serikali za mitaa kutowahamasisha wakazi wao umuhimu wakujiandikisha,.
Mwandishi wa NIPASHE alipita katika vituo hivyo na kushuhudia waandikishaji ambao ni walimu wa shule za msingi wakilalamikia kuwa watu wanakwenda kujiandika baada ya vito kufungwa.
Vurugu nyingine zimeripotiwa kutokea katika Kata ya Manzese ambazo zilianzishwa na mawakala wa vyama, lakini baada ya majadiliano zilisitishwa.
Hivi karibuni, Serikali iliwaagiza wakuu wote wa halmashauri za manspaa na wilaya kusimamia kuhakikisha zoezi la kujiandikisha halifanyiki karibu na maeneo yoyote yanayotoa huduma za kijamii yakiwamo ya hospitali, shule.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, alisema viongozi wawe makini katika zoezi hilo ili kuondoa misuguano baina ya serikali na wananchi kwa sababu wanapokwenda sehemu husika kwa ajili ya kupatiwa huduma.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment