Kikao cha Bunge kinaendelea Dodoma leo Novemba 25, kuna Wabunge ambao waliomba miongozo kwamba suala la mjadala wa Escrow limefikishwa Mahakamani, ambapo walilalamika kwamba kitendo hicho kitazuia Bunge kujadili kuhusu Ripoti ya CAG ambayo iko mikononi mwa kamati ya PAC.
Kutipia mtandao wa Twitter kituo cha ITV (@ITVTANZANIA) kiliripoti taarifa ilisoeomeka hivi;-
“
“
Mbunge John Cheyo aliuliza kuhusu suala hilo; “…Tumepata
taarifa kwamba jambo ambalo Bunge lako linashughulikia sasa,
linapelekwa Mahakamani na dhana ya kuzuia Bunge hili lisifanye kazi
yake. Sasa watu wengine kwa ujanja ujanja wanalipeleka Mahakamani ili
Bunge hili lisifanye kazi yake, hata kama hujapokea hizo taarifa niko
tayari kukupelekea kwa baadaye ili uweze ukatoa mwongozo unaostahili…”
Spika Makinda akajibu; “…Nyie
waheshimiwa Wabunge msianze kuishi kwa wasiwasi, sisi kinga zetu ziko
wazi hakuna mtu anayeweza kutushtaki sisi tusifanye kazi yetu, hayupo.
Hayupo mtu atakayezuia sisi tusifanye kazi za Kibunge na kazi ambazo
zinatokana na kazi zinazopatikana katika maeneo mnayopita. Kwa hiyo,
hiyo shughuli haipo hatuwezi kushtakiwa na nitagawa ile Ripoti
niliyosema nitawagawieni humu ndani kwa majina, Ripoti ya Mkaguzi
itagawiwa humu ndani kwa majina…”
Kusikiliza mjadala huo, nimekurekodia, unaweza kusikiliza hapa mtu wangu.
إرسال تعليق