Hiace iliyopata ajali ikiwa eneo la tukio huku ikiwa
imeharibika vibaya-Picha na Kadama Malunde
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
|
Gari ikiondolewa eneo la tukio
|
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akiwa na maafisa wa polisi mkoa wa Shinyanga eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde |
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
|
Watu watano wanadaiwa kupoteza maisha leo majira ya saa tano asubuhi baada ya gari
ndogo Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikitoka Kahama kwenda Shinyanga
Mjini kupinduka katika eneo la Kona ya Buhangija mjini Shinyanga.
Walioshuhudia wanasema hiace hiyo ilikuwa katika mwendo
kasi ikifukuzana na Hiace nyingine ndipo ikamshinda dereva wake baada ya kupiga
Bamz ya Buhangija na kupinduka mara tatu.
Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema wameondoa miili mitano
ya marehemu katika gari hiyo.
Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa
Shinyanga.
Tutakuletea taarifa kamili hivi punde kuhusu idadi
kamiliya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo na idadi ya majeruhi.
picha na malunde blog
إرسال تعليق