
Mmoja kati ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania akitoa fedha kutoka
katika akaunti yake kupitia mashine ya ATM iliyopo katika tawi jipya la
Benki hiyo la Ushirika lililopo katika Mtaa wa Lumumba jijini Dar es
Salaam jana
======== ======== =========
BENKI
ya Exim Tanzania imeendelea kutanua wigo kwa wateja
wake nchini kwa kufungua tawi jipya lililopo katika mtaa wa Lumumba
jijini Dar es Salaam, ikiwa ni jitihada za Benki hiyo kutoa huduma bora
za kibenki kwa kuwafikia wateja wake wote kiurahisi. Tawi hilo la
Ushirika linaongeza idadi ya mtandao wa matawi ya Benki ya Exim ambayo
yameendelea kusambaa nchi nzima.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi jijini Dar es
Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Operesheni wa Benki ya Exim, Bw. Eugen
Masawe alisema kuwa tawi hilo jipya linaipa fursa nyingine benki ya Exim
kutoa huduma zake za kipekee za kibenki kwa idadi inayozidi kuendelea
kuongezeka ya wateja wake.
“Tunayofuraha kutangaza kuwa Tawi la Ushirika sasa
limefunguliwa rasmi. Hili ni eneo muhimu kwa wateja wetu, kutokana na
urahisi wa upatikanaji wa huduma,” alisema Bw. Masawe.
Alisema kuwa tawi hilo jipya ni uthibitisho pekee wa ukuaji
thabiti wa biashara ya benki yake, ongezeko la idadi ya wateja na
jitihada zake za kutoa huduma za kipekee kwa wateja wake na jamii yote
ya biashara nchi nzima kwa ujumla.
“Tumekuwa
na mkakati wa kumuweka mbele mteja, ambayo umetuwezesha kupeleka huduma
zetu pale ambapo pana wingi wa wateja wetu. “Dar es Salaam kwa kuwa
kitovu cha biashara Tanzania,
tumeshuhudia ongezeko la wateja wengi ambao uhitaji huduma zetu katika
mkoa huu. Tukiwa na matawi zaidi ya kumi jijini, pamoja na huduma mbali
mbali za kibunifu, benki ipo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wateja
wake wanakabiliana na ubize wa ratiba zao kwa kupata huduma za haraka na
bora za kibenki kutoka Benki ya Exim,” alisema Bw. Masawe.
Alibainisha kuwa jitihada hiyo ya benki kutanua wigo wake
haitoongeza tu mizania ya benki yake kwa kiasi kikubwa na kuongeza idadi
ya wateja wake, lakini pia kuhakikisha kuwa benki inayafikia masoko
mengine ambayo bado hayajafikiwa nchini. “Tunampango wa kuendelea kufungua matawi mengine nchi nzima
katika siku za usoni. Utekelezwaji wa mkakati huo utaiwezesha benki ya
Exim kupeleka huduma zake karibu zaidi na wateja wake,” aliongeza.
Post a Comment