![]() |
| Jaji Werema |
MWANASHERIA
Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema amewataka Mawakili wa Serikali Wafawidhi
wa mikoa na Wilaya kufuata kanuni na taratibu ili kuhakikisha kesi za
Madawa ya Kulevya na Uhujumu Uchumi zinakamilishwa haraka na haki inatendeka.
“Kuna
mambo mengi yanaharibu taswira ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuna
malalamiko kwamba hatufanyi vizuri katika uendeshaji wa kesi za Madawa ya
Kulevya na Kesi za Uhujumu Uchumi. Hatuna sababu za
kujitetea. Tunachopaswa kufanya ni kujisahihisha na kuwa makini wakati
tunaposoma majalada ya upelelezi na kuamua kufungua mashtaka.” alisema
Aliwataka
kuhakikisha wanatumia weledi wa uwakili katika kuwashauri wapelelezi ili
kuwaongoza katika kupata ushahidi utakaowezesha makosa ya jinai kuthibitika
Mahakamani
Jaji
Werema alitoa kauli hizo jana wakati akifungua mkutano wa mawakili wa serikali
wafawidhi wa mikoa na wilaya.
Alisema
wakiwa kama viongozi wana wajibu wa kuwaelekeza na kuwasimamia watumishi walio
chini yao na kila mtumishi anapaswa kuzingatia nidhamu mahali pa kazi kwa
kufuata Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayosimamia utumishi wa umma.
“Kuna
malalamiko kuwa baadhi mnajihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo
kuchelewa kazini, ulevi, kuvaa mavazi yasiofaa, kufuta kesi bila kufuata
utaratibu, kutojiandaa vyema kabla ya kuendesha mashauri mahakamani,
kutoishauri ipasavyo mahakama katika misingi ya haki; na kujihusisha na vitendo
vya rushwa” alisema
Alisema
kuna taarifa baadhi yao hawatumii nafasi ya kusoma maoni ya Mawakili
vizuri na sehemu nyingine hakuna maoni ya awali ya kushtaki au kutoendelea na
mashtaka na hiyo ni kasoro kubwa na ukiukwaji wa maadili ya kazi ya Uwakili wa
Serikali.
Jaji
Werema alisema kuna umuhimu wa kuweka na kutunza kumbukumbu, taarifa na takwimu
sahihi kuhusu utendaji kazi kwani maoni ya awali ni moja ya kumbukumbu muhimu
za kutambua weledi wa Mawakili; kujua sababu za kufungua mashtaka au
kutoendelea na mashtaka; maoni haya yanarahisisha uendeshaji wa mashtaka kwa
yeyote atakayepewa kazi ya kuendesha mashtaka hayo. .
Aliwaonya
kuacha kutoa siri za serikali kwani mara nyingi wamejikuta wakishiriki kwenye
mitandao ya kijamii bila kujua wanatoa siri za serikali.
“Baadhi
yenu mmekuwa mkichangia kwenye mitandao ya kijamii bila kujua mnatoa siri za
serikali. Nyie si wasemaji wa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali” alisema.
Pia
aliwataka Mawakili wa Serikali Wafawidhi, Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi
kumpa ushirikiano Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga ambaye aliteuliwa
na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni ili aweze kutekeleza majukumu yake vyema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mashitaka, Biswalo Mganga alisema dhumuni la mkutano
huo ni kujadili kwa pamoja na kufanya tathimini ya mafanikio na changamoto
wanazopata katika utekelezaji wa majukumu ya divisheni ya mashtaka na mawakili
wa Serikali na ofisi zote za Mikoa na Wilaya.
Alisema
uvujaji wa siri za serikali umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwa sababu hiyo na
kuangalia asili ya kazi wanazofanya wanapaswa kuwa waangalifu zaisi ili
kutojiingiza katika mazingira yoyote yatakayohatarisha usalama wa ofisi zao.
Alisema
kutokana na hayo utunzaji wa majalada uteketezwaji wa nyaraka zisizohitajika,
mawasiliano na habari za ofisi na mamno mengine yote yanatakiwa yafanyike kwa
kuzingatia sheria, utaratibu na kanuni zinazowaongoza.
Aliwataka
kujikumbusha sheria ya usalama wan chi namba 3/1970 kuhusiana na masuala ya
utunzaji siri za ofisi.
Source:
Sifa Lubasi, HabarileoDodoma

Post a Comment