
Mwili
wa marehemu aliyefahamika kwa jina moja la Betty baada ya kupigwa
risasi leo asubuhi huko Yombo Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam akiwa
kwenye gari aina ya Toyota Pick Up mali ya Tunu Security na watu
waliokuwa katika bodaboda.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Mwili wa marehemu Betty ukibebwa na polisi kupelekwa Hospitali ya Chang'ombe, Dar kwa uchunguzi.
...Polisi wakiweka mwili wa marehemu ndani ya gari.
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari.
Mtu asiyefahamika (mwenye simu katikati) akiwasiliana na ndugu wa marehemu Betty baada ya kufika eneo la tukio.
DADA aliyefahamika kwa jina moja la Betty ameuawa kwa kupigwa risasi leo
saa mbili asubuhi maeneo ya Yombo-Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam
akiwa kwenye gari aina ya Toyota Pick Up mali ya Tunu Security.
Marehemu Betty ameuawa na watu waliokuwa kwenye bodaboda wakati akiwa
kwenye gari la Tunu Security akitokea kituo cha mafuta kuelekea benki.
Watu hao waliokuwa kwenye bodaboda mmoja alimpiga dereva wa gari risasi
ya mkononi alafu akampiga Betty risasi ya kichwani huku mlinzi aliyekuwa
katika gari hilo akikimbia ambapo watu hao walichukua mfuko uliokuwa na
pesa na kutokomea kusikojulikana.
Baadaye mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi na kupelekwa Hospitali ya Chang'ombe,Dar kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
(PICHA NA GPL
Post a Comment