Boko Haram waua wachuuzi 48 wa samaki Nigeria

Wanamgambo wa kitakfiri wa kundi la Boko Haram wa huko Nigeria wamewauwa wachuuzi wa samaki wasiopungua 48 huko katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. 

Hayo yemeripotiwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Samaki ya Nigeria. 

Abubakar Gamandi, Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Samaki ya Nigeria amesema leo kuwa wahanga wa mauaji hayo waliuawa baada ya wanamgambo wa Boko Haram kuweka kizuizi barabarani katika eneo la Dagon Fili na kusimamisha msafara wao Alkhamisi iliyopita.

Kwa mujibu wa Gamandi, makumi ya wanamgambo wa Boko Haram siku ya Alkhamisi walizuia njia inayounganisha Nigeria na Chad karibu na kijiji cha uvuvi cha Doron Baga katika ufukwe wa Ziwa Chad na kuuwa kundi la wachuuzi wa samaki 48 waliokuwa wakielekea Chad kununua samaki.

Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Samaki ya Nigeria amesema kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliwauwa wachuuzi kadhaa wa samaki na kuwatupa wengine ziwani ili wazame baada ya kuwafunga mikono na miguu yao ili wasiweze kuogelea.

Post a Comment

Previous Post Next Post