
Ofisi ya CHADEMA mkoa wa Singida katika picha.
Na Nathaniel Limu, Singida
WAKATI
siku zikishika kasi kuelekea uchaguzi mkuu mwakani,’Bundi’ ametua
ndani ya CHADEMA mkoa wa Singida,na hali imechafuka kwa viongizi wake
kuanza kuvuana uanachama na kufukuzana uongozi.
Baraza
la uongozi mkoa wa Singida, limemvua na kumfukuza uongozi Mwenyekiti wa
jimbo la Singida mjini,J ohn Kalaye Kumalija kwa tuhuma ya kuwa na
mgogoro wa muda mrefu na katibu wake.
Uamuzi huo umeaanza kutekelezwa kuanzia Oktoba saba mwaka huu.
Hayo
yamo kwenye barua iliyoandikwa na Katibu baraza la uongozi mkoa wa
Singida,Patrick Mssuta ya Oktoba saba mwaka huu, isiyokuwa na
kumbukumbu.
Aidha,kwa
mujibu wa baraua hiyo (mwandishi wetu anazo nakala zake) inadai
Mwenyekiti huyo alifanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kugombana
hadharani na Katibu wake Yahaya Ramadhan.
Kutokana
na uamuzi huo,baraza la uongozi mkoa wa Singida,limemwagiza Kumalija
kukabidhi ofisi mara moja kwa katibu mwenezi wa jimbo,mwenyekiti wa
baraza la wazee au kamati ya utendaji ya jimbo.
“Pia
unatakiwa kutojishughulisha na shughuli za uongozi au za chama kwa muda
huu ukiwa chini ya uangalizi maalum wa chama”, imesema barua hiyo.
Hata
hivyo,Katibu Mssuta katika barua yake hiyo, amejichanganya baada ya
kichwa cha habari kusomeka kuwa Kumalija anasimamishwa uongozi, halafu
ndani ya maelezo yake,amesema baraza la uongozi mkoa,limemvua na
kumfukuza uongozi.
Kwa upande wake Kumalija,amejibu mapigo,kwa barua yake ya Oktoba 31 mwaka huu ambayo nayo haina kumbukumbu.
Katika barua yake,Kumalija amedai kuwa hana mgogoro wowote na katibu wake Yahaya Ramadhan.
“Baraza
lako halina mamlaka yo yote ya kunisimamisha na kunivua uongozi.Mamlaka
ya kuchukua/kutoa maamuzi hayo ni mkutano mkuu wa wilaya au
jimbo,Kumalija amesema na kuongeza;
“Kwa
sababu hizo na zingine,Mimi John Kalaye Kumalija,najitambua kuwa bado
ni mwenyekiti halali wa CHADEMA jimbo la Singida mjini”.
Post a Comment