
Katibu
Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, akizungumza kwenye ufunguzi wa
semina juu ya kuongeza upatikanaji wa mbegu bora na mbolea kwa wakulima
wadogo wadogo kwa kuimarisha masoko ya pembejeo katika mikoa ya Singida
na Dodoma.
Na Nathaniel Limu, Singida
KATIBU
tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, amewahimiza wadau mbalimbali
wanaojishughulisha na sekta ya kilimo,kuweka mikakati ya kuhakikisha
zaidi ya aslimia 85 ya wakulima wawe wanatumia mbegu bora,ili kuleta
mapinduzi ya kweli ya kilimo na kuwa cha kibiashara zaidi, katika mikoa
ya Singida na Dodoma.
Hassan
alisema mapinduzi hayo ya kilimo cha kibiashara, yaweze kuwatoa
wakulima kwenye kilimo cha kujikimu ambapo kwa sasa matumizi ya pembejeo
bora ni chini ya aslimia 40 tu.
Katibu
tawala huyo aliyasema hayo wakati akifungua warsha ya siku mbili
iliyohusu kuongeza upatikanaji wa mbegu bora na mbolea, kwa wakulima
wadogo wadogo kwa kuimarisha masoko ya pembejeo mikoa ya Singida na
Dodoma.
Akiijengea
nguvu hoja yake hiyo, alisema ili kupandisha kiwango hicho cha kutoka
asilimia 40 hadi zaidi ya aslimia 85 watakao tumia pembejeo
bora,kunahitajika kuwajengea uwezo zaidi mawakala na kuzidi kuongeza
idadi ya majaribio.

Baadhi
ya wakulima wadogo wadogo mkoa wa Singida na Dodoma,wakifuatilia mada
zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya siku mbili iliyohusu kuongeza
upatikanaji wa mbegu bora na mbolea.(Picha na Nathaniel Limu).
Katika
hatua nyingine Katibu tawala huyo, alitumia fursa hiyo kulipongeza
shirika la FIPs Africa (farm input promotion) kwa mfumo wao wao
kuwafikia wakulima kwa kuwahamasisha kutumia njia mbalimbali za matumizi
bora ya pembejeo.
“Kwa
kipindi hiki chote nimeambiwa kuwa FIPs kwakushirikiana na halmashauri
zetu,wamejenga mtandao wa wakulima ambao wamejiajiri wenyewe kupitia
kuuza mbegu na kuchanja kuku”,alisema katibu huyo.

Akifafanua
zaidi,Hassan alisema kuwa FIPs hawakuishia hapo,bali pia wamewasaidia
wakulima wa mkoa wa Dodoma na Singida kuboresha udongo,kuboresha
mazingira na hatimaye kuwezesha mkoa hii kujitosheleza kwa chakula.
“Pia
nimeambiwa kuwa kupitia warsha hii, mtafanya mapitio ya shughuli ambazo
zimefanyika tangu mradi huu uliopoanza.Ni imani yangu kwamba mapitio
hayo yatawasaidia kutengeneza mpango kazi na mapendekezo yatakayosaidia
kuendeleza kufanya shughuli zilizoanzishwa baada ya mradi huu kumaliza
muda wake”,alisema Hassan.
Post a Comment