Diamond Platnumz anyakua tuzo tatu za #CHOAMVA14 - Wajue Hapa Watu wengine walionyakua Tuzo Hizo Pia

November 29, haitakumbwa kwenye maisha ya Diamond Platnumz na familia yake pekee, bali pia kwenye muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, baada ya hitmaker huyo wa ‘Number One’ kunyakua tuzo tatu kwenye tuzo za Channel O.
10448985_756780187704186_1932636597_n Diamond, Salam, Babutale na Vanessa Mdee wakiwa na tuzo
Diamond alikuwa ametajwa kwenye vipengele vinne. Vipengele hivyo ni pamoja na Most Gifted East Video, Most Gifted Afro Pop Video na Most Gifted Newcomer.
Kwenye tuzo hizo Diamond amefanikiwa kuwapiku wasanii nguli wa Afrika wakiwemo Iyanya, Davido, Flavour, Mafikizolo na Sauti Sol.
Ushindi huo umepokelewa kwa furaha kubwa na Watanzania wakiwemo wasanii wenzake.
“@diamondplatnumz wow congrats bro 3rd award already!! #cocobaby,” ameandika msanii wa Nigeria, Waje.
Hitmaker wa Doc Shebeleza, Casper Nyovest naye amenyakua tuzo tatu, Most Gifted South Video, Most Gifted Male Video Doc na tuzo kubwa ya usiku huo, Most Gifted Video of the Year.
Hii ni orodha nzima ya washindi:
Most Gifted Video of the Year
Doc Shebeleza – Casper Nyovest

Most Gifted Male Video
Doc Shebeleza – Casper Nyovest

Most Gifted Female Video
Eminado – Tiwa Savage

Most Gifted Afro Pop Video
Number One – Diamond Platnumz

Most Gifted South Video
Doc Shebeleza – Casper Nyovest

Most Gifted East Video
Diamond

Most Gifted West Video
‘Turn Up’ – Olamide

Most Gifted duo/group/featuring
Pull Over – KCEE f/ Wizkid

Most Gifted Kwaito
Uhuru ft Oskido & Professor

Most Gifted RnB Video
‘Crazy But Amazing’ – Donald

Most Gifted Hip hop Video
Congratulate – AKA

Most Gifted Dance Video
Ngoku – Busiswa

Most Gifted Newcomer
Diamond Platnumz

Most Gifted Ragga Dancehall
Buffalo Souljah

Post a Comment

Previous Post Next Post