VYUMBA VITATU VYATEKETEA KWA MOTO DAR


Askari wa zimamoto wakiwa kazini. Sehemu ya ukuta ilivyoungua. mmoja wa wanafamilia akikagua kama kuna kilichosalia. Mtungi huu wa gesi ndiyo ulisalimika peke yake katika vyumba hivyo vitatu. Vitu vilivyosalimika katika baadhi ya vyumba baada ya kuwahi kuvitoa. Moja ya chumba kilichonusurika kuungua. Ndugu na majirani wakijadili jambo.
FAMILIA moja iliyopo maeneo ya  uwanja wa Tip Sinza, jijini Dar es Salaam, imejikuta ikipata wakati mgumu baada ya vyumba vitatu walivyokuwa wanaishi kuteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.
Wakizungumza na GPL kuhusu chanzo cha moto huo, wanafamilia hao walisema  ni kutokana na shoti ya umeme iliyoanzia kwenye swichi, huku jeshi la polisi kitengo cha zima moto likitupiwa lawama kwa kuchelewa kufika eneo la tukio.
Mmoja wa askari wa zimamoto aliyezungumza na GPL (jina linahifadhiwa kwa kuwa si msemaji) alisema walipata taarifa saa 4 asubuhi kutoka polisi, na wakati moto huo ulianza majira ya saa 3 asubuhi kwamba walifika eneo la tukio saa 4:21.
Aidha walisema pamoja na kujitahidi kuwahi lakini bado changamoto zinawakabili zikiwemo miundombinu, ubovu wa barabara na foleni.Tembelea www.globaltvtz.com ili kujua mengi zaidi katika ajali hiyo.
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha na Mayasa Maliwata/GPL)

Post a Comment

Previous Post Next Post