Wakizungumza na GPL kuhusu chanzo cha moto huo, wanafamilia hao walisema ni kutokana na shoti ya umeme iliyoanzia kwenye swichi, huku jeshi la polisi kitengo cha zima moto likitupiwa lawama kwa kuchelewa kufika eneo la tukio.
Mmoja wa askari wa zimamoto aliyezungumza na GPL (jina linahifadhiwa kwa kuwa si msemaji) alisema walipata taarifa saa 4 asubuhi kutoka polisi, na wakati moto huo ulianza majira ya saa 3 asubuhi kwamba walifika eneo la tukio saa 4:21.
Aidha walisema pamoja na kujitahidi kuwahi lakini bado changamoto zinawakabili zikiwemo miundombinu, ubovu wa barabara na foleni.Tembelea www.globaltvtz.com ili kujua mengi zaidi katika ajali hiyo.
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha na Mayasa Maliwata/GPL)
إرسال تعليق