Diamond Platnumz kuingia kwenye jumba la BBA Hotshots leo (Nov 27) kupiga story na washiriki

Diamond Platnumz tayari ametua jijini Johannesburg, Afrika Kusini toka jana, tayari kuhudhuria tuzo za Channel O (CHOAMVA) zinazotarajiwa kutolewa siku ya Jumamosi Nov.29 akiwa anawania vipengele vinne.
diamond2
Staa huyo ambaye ameachia ngoma mpya siku chache zilizopita ‘Ntampata wapi’, ameandika kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamaii kuwa pia leo Alhamisi Nov.27 atapata nafasi ya kuingia kwenye jumba la Big Brother kubadilishana mawazo na washiriki.
“Tafadhali usikose kuangalia Big Brother Afrika kuanzia saa tano Asubuhi kesho (leo), kijana wako Platnumz ntakuwa ndani ya nyumba nikizoza mawili matatu na washiriki….” aliandika Diamond.

Post a Comment

أحدث أقدم