Mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu,
mwanadada Faiza Ally ameamua kuwatolea uvivu watu wanaodai kuwa
ameachwa na mheshimiwa huyo kutokana na mavazi yake.
Faiza ambae ana mtoto na Sugu, katika instagram ameandika:
“Sasa leo ngoja nifunguke…. Yaani nikiweka picha zangu kwa raha zangu
mnaanza kusema oh ndio maana SUGU kakimbia ndio maana kaniacha Nasema
hivi MIMI NDIO NIMEMUACHA mkome kunisema nimeachana na nimemuacha tukiwa
kwenye process za ndoa na tulisha kutana na padri na kwenye jumuiya
nilisha anza ….. Kuna vitu vikinifanya niondoke kabla ya ndoa ambavyo
vitabaki kuwa vya kifamilia ……. Nyie mna muona sugu Kama si mtu wa
kawaida mm namuona Kama alie kuwa mpenzi wangu na Sasa ni baba wa mtoto
wangu …. Lkn anajua ubora wangu na faida zangu Pumbavu zenu nyote mnao
zani niliachwa tena kwa mavazi anajua na anapenda mavazi yangu …..
Nachukia kuamka asubuhi na kukuta comments za kusemwa vibaya…. Nyie
mnajua tabia zake ????? Au mnamuona kwa mbali ?????”
إرسال تعليق