ESHA BUHETI AOGOPA DHAMBI YA KUJICHORA TATUU

Stori: Imelda Mtema
MSANII wa filamu za Kibongo, Esha Buheti, amesema kuwa anaweza akafanya vitu vingi vya kujiremba lakini anaogopa sana kujichora tatuu kwani ni dhambi.

Msanii wa filamu za Kibongo, Esha Buheti.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii,  Esha alisema kuwa kitu ambacho anahisi inaweza kuwa ni moja ya dhambi mbaya kabisa ni kujichora tatuu mwilini kwani katika dini yoyote au dhehebu lolote halikubali mtu kujichora vitu tofauti na uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
“Nitaiga vitu vingine kama mavazi na hata nywele lakini siyo kujichora tatuu katika mwili wangu maana ni vitu hatari sana na vinakatazwa kabisa katika dini yangu ya Kiislamu,” alisema Esha.

Post a Comment

أحدث أقدم