Coutinho awaletea Simba... beki Mbrazili

Kiungo wa Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho.
Na Said Ally
KIUNGO wa Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho, ameushauri uongozi wa Simba katika kipindi hiki cha usajili, iende nchini humo kusajili beki hatari.Coutinho yupo nchini kwao kwa ajili ya mapumziko ya siku 10 waliyopewa na uongozi wa timu hiyo baada ya kusimama kwa ligi.

Akizungumza na Championi Jumatatu moja kwa moja kutoka Brazil, Coutinho alisema kama viongozi wa Simba wanatafuta wachezaji imara ambao wataisaidia timu hiyo, anawashauri waende nchini humo kutokana na kujaa wachezaji wengi wenye vipaji.
“Nilikuwa nawashauri viongozi wa Simba waje nchini Brazil kusajili wachezaji ambao watawasaidia, kwani kuna wachezaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu.“Mpaka sasa kuna beki mmoja ameweka wazi nia yake ya kutaka kuja Tanzania kucheza soka la huko na kama timu hiyo itafanikiwa kumnasa, itakuwa imepata ‘jembe’ kutokana na staili yake ya ukabaji,” alisema Coutinho.
Msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Yanga ndiyo timu pekee yenye wachezaji raia wa Brazil ambao ni Coutinho na Geilson Santos ‘Jaja’ ambaye hata hivyo ameomba kutorudi nchini kutokana na matatizo ya familia huku nafasi yake ikichukuliwa na kiungo mkabaji, Emerson.

Post a Comment

أحدث أقدم