Exclusive: Diamond afunguka kuhusu Wema, Zari, Penny, Chameleone, Yemi Alade, Waje na mengine (Video)

Tumekaa na Diamond Platnumz kuzunguma mambo kibao hususan tetesi zinazoendelea sasa kuwa ameachana na mpenzi wake Wema Sepetu na kuwa ana uhusiano na mfanyabiashara mrembo wa Uganda, Zari the Bosslady pamoja na issue zingine. Itazame hapo chini au soma kwa kifupi baadhi ya kile alichokisema.

Kuhusu kwanini anatumia wazungu zaidi kwenye video zake
Mimi nafikiri ni kutokuwa na uelewa tu kwasababu inategema na concept. Ukiangalia kama ‘Mdogo Mdogo’ ilikuwa inazungumzia mapenzi hayaulizi kwanini so ilikuwa lazima ioneshe pande mbili, kuna wazungu na mimi ni mwaafrika na familia yangu ya kiafrika. Kuna mtoto wa kizungu ambaye ananizimia mimi mwaafrika lakini familia yake haipendi ukizingatia wao ni wafalme na nini. Lakini mtoto bado ananipenda hivyo hivyo, ananifuata mpaka porini ananikuta kwenye maji naimba mimi kule. Mpaka dakika ya mwisho anakuja baba yake anamkuta yupo kwetu kijijini anacheza na familia yetu sisi so dakika ya mwisho unakuta mzee mwenye anakubali mwanae aolewe.
Sasa huwezi kufanya familia ya kiafrika na familia ya kiafrika, haiwezi kuleta maana, lazima iwe tofauti. Ukiangalia kama video ya ‘Ntampata Wapi’ watu wanashindwa kuelewa, yule model sio mzungu. Ni mwaafrika sababu anaishi south kaiva sana. Ukiangalia kuna waafrika, kuna wazungu.. unajua ukiwachanganya inakufanya uweze kuwavuta na watu wengine waconcentrate na ile nyimbo, waone kama hata sisi inatuhusu, usifanye issue za kibaguzi.
Kuhusu anavyomchukulia model wa kwenye video ya Ntampata Wapi, Melissa
2
Kiukweli amejitahidi na amefanya vizuri sana. Bado tunawasiliana, hata juzi nilimtumia meseji nikamwambia ‘Melissa natamani ujue jinsi gani unazungumziwa, nikasema ‘najua kabisa huko South Africa hawawezi kuwa wanaizungumzia hii video kama wanavyoizungumzia hii video huku nyumbani, natamani ujue jinsi gani walivyokupokea, natamani ujue umefahamika kiasi gani. Nikamwambia ‘siku ntakutag Instagram, halafu utaona shughuli yake.’ Ntamuweka siku moja Instagram, najua watu wanasubiri akaunti yake.
Kuhusu kufanya kazi na Yemi Alade kwenye kipindi cha Coke Studio Africa
Kiukweli mimi nafikiri ilikuwa ni kama zari. Kitu ninachompendea Yemi Alade kwanza yeye mwenyewe ni mtu mwendawazimu fulani akifika kwenye stage, ni chizi muziki, akifika kwenye muziki anakuwa hana haya. Unaweza ukatoa pande la haraka haraka ‘mwanangu tugonge hivi, akagonga’ ni mtu wa miongezeko na yuko charming.
Kuhusu remix ya wimbo ‘Kissing’ wa Yemi ambao Diamond alishirikishwa
Kuna vitu fulani ilitakiwa virekebishwe kwasababu Yemi aliniambia atakuja Tanzania kwasababu tufanye video ya ile remix , kuna njonjo fulani zinatakiwa ziongezeke, so alikuwa na plan ya kushoot video ya remix, nikamwambia ‘that’s a good idea.
Kuhusu tetesi kuwa ameachana na Wema Sepetu
Unajua mahusiano ya umaarufu yana mazuri na madhara yake, so lazima uwe na akili ya ziada kuweza kujua unazungumza vipi kuhusu masuala yenu na unaweza vipi kuhandle mambo yenu, either kwenye mambo mazuri au mabaya. Ndio maana kuna vitu vingine vinafaa kuwa vinatoka, vingine vinakuwa havifai. So situation iliyopo kuanza kuisema katika media ikiwa haikuwa tayari inakuwa sio vizuri kwasababu mtu anaweza akakutafsiri vibaya mwingine akakuona kama unaongea sana, hauna roho ya kiume. So kuna vitu fulani ambavyo lazima viwe na muda muafaka kwamba najua huu muda sasa hivi vinaweza kuweka hadharani na watu wakasikia, najua watu wanataka kusikia, watu wanatamani kusikia kauli kutoka pande zote.
Kuhusu picha ambayo yeye na Zari the Bosslady wanaonekana wakipigana busu
Unajua kwenye movie kuna watu wanakuwa kabisa kama wanakulana, hawana nguo kabisa so ukiangalia kwa mtazamo mfupi unaweza ukaona kabisa hawa walikuwa wanamegana, that’s what we said before, it’s a project, project inabeba vitu vingi ndani yake. Unajua ilikuwa rahisi kutoka mwanzo kuzungumza kwamba project yenyewe ni hii na hii, lakini sasa ukisema unakuwa unaua kick ya project. Lazima watu waisubiri kwa hamu, kwa heshima na taadhima kama inadondoka lini, ila nafikiri muda wake umebaki mchache sana.
Kuhusu Wema Sepetu na Penny kupatana

Mimi nafikiri ni kitu kizuri. Wanapokuwa wanapatana kwanza inakuwa ni heri inatengeneza njia na mifano bora hata kwa wanawake wengine kufuta zile zama za kijinga na maneno ambayo yalikuwa yakiandikwa. Kwahiyo mimi nafurahi, halafu ukizingatia mimi ni muislamu naweza nikaoa wanawake wanne.
Kuhusu kama yeye na Penny hawapatani tena
Kiukweli sijawahi kupotezeana na Penny kabisa, ni mwanangu sana, nisiwe mnafiki. Hata hapa katikati alikuwa akinipa deal nyingi sana za kazi na nini. Ni mwanangu yaani, mimi namuitaga ‘Aunt Penny’, na yeye ananiitaga ‘Uncle Chibu.’
Kuhusu taarifa kuwa Jose Chameleone alimuomba collabo
Kwanza nilipoona kimeandikwa, kilinisikitisha, lakini kwasababu naiheshimu Bongo5 sikuweza kuikanusha. Ni story ambazo si za ukweli. Mimi na Chameleone ni mtu ambaye huwa tunazungumza vitu vya kimaendeleo. Nakumbuka mawasiliano yangu na Jose nilimwambia ‘Jose mimi nakuheshimu sana kwasababu aliniambia ‘unafanya vizuri sana mdogo wangu’ nikamwambia ‘nashukuru lakini jua nakuheshimu sana, kwasababu mimi nimeanza kukusikia sijui nitatoka lini.
Mpaka leo mimi ninatoka, nakukuta bado unafanya vizuri’. Nikamwambia ‘Bro hongera sana mimi nimeshaona watu wengi sana wanakuja, wanatoka wanaondoka’. Yaani nilimwambia ‘kaa ukijua mimi nakuheshimu sana,’ so huwa nachat naye vizuri tu. Ilivyotokea ile issue, nakibaki ‘sijui nafanya vipi’ Nikasema nikianza kumtext Jose, atanihisi kama najishtukia, ikabidi nikae kimya. Juzi kati akanitafuta Profesa, akaniambia ‘nina ujumbe wako kutoka kwa Jose, akaniambia ujumbe wako ‘ni hivi na hivi’. Sasa mimi nikamwambia ‘bro, mimi kinachonisikitisha Jose ni mtu ambaye mimi ninaongea naye, tena nikiongea naye naongea kwa heshima na taadhima, ameshindwa vipi kunitext au kunuambia, mdogo wangu hili suala likoje? Kwanini hajaniambia! Nina kila sababu ya kumheshimu Jose, kwanza kanizidi umri, kanizidi kimaendeleo, kwahiyo kikitokea kitu halafu akikichukulia moyoni, bila kuniambia naona haiwezi kwenda hivyo.
Kuna kampuni inaitwa Mziiki ambayo mimi ni balozi na Jose pia ni balozi wa Mziiki ambapo inakiwa tufanye wimbo wa Mziiki lakini hatujakaa kuzungumza labda Jose kuniambia ‘nataka tufanye collabo. Hata tukizungumza masuala ya kufanya nyimbo, hatuzungumzii kwamba kuna mtu kwamba anataka msaada au anataka booster, kiukweli hizi habari zimenisikitisha sana. Na mimi sio kwa kufikiria tu, nina imani lazima kutakuwa na watu wananichonganisha sana na Jose. Kwasababu kuna kipindi katikati aliniblock kwenye Instagram. Nikamwambia ‘mbona sikupati bro’ kwasababu najua kuna watu wengi wanaweza kumpelekea mambo mabaya mabaya ya kutaka anichukie mimi. Lakini kiukweli mimi sijazungumza kauli hizo, hata kama Jose atakuwa anatazama, ajue hivi ni vitu vya uongo na vitu ambavyo vinatungiwa. 
- Bongo5

Post a Comment

Previous Post Next Post