Stori: Erick Evarist na Imelda Mtema JAHAZI
linazidi kwenda mrama! Wakati shauri lao la kugawana mali likidaiwa
kufikishwa mahakamani, picha mpya imenaswa ikionesha dhahiri kwamba
Mtangazaji Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteni’ ameamua kusonga
mbele na maisha yake na kusahau kabisa kama alikuwa na mke aitwaye
Judith Daines Wambura Mbibo ‘Jide’, Amani linakupa mchapo kamili.
Mtangazaji
Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteni’ akila ujana na binti (jina
halikupatikana mara moja) mrembo bwawani (swimming pol).
PICHA IPOJE?Picha hiyo ambayo inamuashia ‘endiketa’ Jide kuashiria kwamba, Gardner amejiweka pembeni na kuwa bize na ‘starehe’ zake, inamuonesha mtangazaji huyo akiwa ‘ziro distensi’ na kabinti kabichiii (jina halikupatikana mara moja) katika bwawa la kuogelea (swimming pol) huku wakiwa wamening’iniza miguu kwenye maji.
PICHA ILIVYOVUJA
Kwa mujibu wa chanzo makini, picha hiyo iliibwa katika simu ya binti huyo aliyekuwa na Gardner kisha kuisambaza katika mitandao ya kijamii bila yeye mwenyewe kujua.
“Yule dada aliyekuwa na Gardner aliibiwa picha hiyo na shosti yake katika simu yake ndipo akaisambaza mitandaoni,” kilisema chanzo hicho.
NI WAPI?
Mara baada ya mapaparazi wetu kunasa picha hizo, kabla ya kumtafuta Gardner ili kujua ukweli, walianza kusaka eneo ambalo wawili hao walikuwa wakiponda raha zao ambapo jitihada hizo zilikosa majibu ya moja kwa moja.
“Hii ilikuwa ni Mikocheni, Escape One siku hiyo kaka mkubwa alikuwa akifanya yake si unajua tena ameshaona liwalo na liwe,” kilisema chanzo cha kwanza.
ETI NI KIGAMBONI
Chanzo kingine kilichozungumza na mapaparazi wetu kilipishana na mwenzake kwa kudai kuwa wawili hao walikuwa katika ufukwe wa Southern Sun Kigamboni wakijiachia kwa raha zao.
“Mimi kuna kuna mtu kanihakikishia kabisa hii ilikuwa ni Kigamboni, walikuwa wakiponda raha tena Gardner siku hiyo inaonekana alikuwa ameonja kidogo si unajua tena kaka mkubwa na mambo yetu yale, Jide hana chake tena pale,” kilinyetisha chanzo kingine.
Chanzo kingine kilichozungumza na mapaparazi wetu kilipishana na mwenzake kwa kudai kuwa wawili hao walikuwa katika ufukwe wa Southern Sun Kigamboni wakijiachia kwa raha zao.
“Mimi kuna kuna mtu kanihakikishia kabisa hii ilikuwa ni Kigamboni, walikuwa wakiponda raha tena Gardner siku hiyo inaonekana alikuwa ameonja kidogo si unajua tena kaka mkubwa na mambo yetu yale, Jide hana chake tena pale,” kilinyetisha chanzo kingine.
Gardner akiwa na Lady Jaydee.
NDIYO ZAKE?Wakati mapaparazi wetu wakiendelea kuchimba data kuhusiana na mtangazaji huyo ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika Kipindi cha Jahazi cha Redio Clouds FM, chanzo kingine kilipenyeza madai kuwa, Gardner kwa sasa ndiyo zake kujiachia na ‘totoz’ tofauti.
“Aaah…kwani nyinyi hamjui? Jiongezeni bwana, Gardner kwa sasa ameshaondoa mawazo kabisa kwa Jide na badala yake anajipoza tu kwa totoz,” kilisema chanzo.
MAKABRASHA YA LIBRARY
Katika makabrasha yaliyopo katika kumbukumbu za Magazeti Pendwa, Gardner aliwahi kunaswa na kabinti kengine katika Fukwe za Coco jijini Dar wakiwa wamegandana kama kumbikumbi.
GARDNER ASAKWA
Mapaparazi wetu juzikati walimfuata Gardner katika Ofisi za EFM zilizopo Mikocheni jijini Dar ambako mtangazaji huyo anafanya kazi kwa sasa, mtu wa mapokezi alidai hajafika.
ATUMIWA UJUMBE
Jitihada za kumpata kwenye simu zilipogonga mwamba, mapaparazi wetu walimtumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kumsomea mashitaka yake na kama ni kweli ameamua kumpotezea mazima Jide.
Gardner hakujibu mapema, baadaye alipigiwa simu, akapokea na kuambiwa ajibu mashitaka yake kama alivyotumiwa katika SMS. Alijibu kuwa yeye ana marafiki wengi hivyo si kila atakayeonekana naye basi ni mpenzi wake. Msikie:
“Hivi kila mdada nitakayeonekana naye atakuwa ni wifi jamani? Mi nina marafiki wa jinsi zote, sina la kusema.”
UKWELI NI NINI?
Mapaparazi wetu walizidi kumtafuta Gardner kujua ukweli wa picha hiyo na eneo walilopigia lakini hakupokea tena hivyo ukweli anaujua mwenyewe.
TUJIKUMBUSHE
Gardner na Jide waliofunga ndoa Mei 14, 2005 na kutobarikiwa kupata mtoto, Agosti mwaka huu walidaiwa kumwagana.
Post a Comment