HAKUNA KAMA LIONEL MESSI LA LIGA …AWEKA REKODI YA KUWA MFUNGAJI MWENYE MAGOLI MENGI KULIKO YEYOTE YULE

Messi (top) is hoisted up high by his Barcelona team-mates after his second goal of the night broke Telmo Zarra's record
Akiwa bado mbichi kabisa katika umri wa miaka 27 tu, Lionel Messi ameandika historia mpya ya kuwa mfungaji mwenye magoli mengi zaidi La Liga, akiwa anavunja rekodi ya mshambuliaji Telmo Zarra.
Zarra akiwa na Athletic Bilbao mwaka 1955 aliandika bao lake la 251, rekodi iliyodumu hadi Jumamosi usiku wakati Messi alipofunga mabao matatu katika ushindi wa 5-1 wa Barcelona dhidi ya Sevilla.
Messi alifunga katika dakika ya 21, 72 na 78 wakati Neymar alifunga dakika ya 48 na Rakitic naye pia akifunga katika dakika ya 65. Bao la Sevilla lilikuja dakika ya 47 baada ya Alba kujifunga.
Barcelona: Bravo, Alves, Pique, Mathieu, Alba (Adriano 80), Busquets, Rakitic, Xavi (Rafinha 77), L Suarez (Pedro 74), Messi, Neymar.
Sevilla: Beto, Coke, Carrico, Pareja, Diogo, Krychowiak, Banega, D Suarez (Gameiro 62), Aleix Vidal (Deulofeu 62), Vitolo, Bacca (Aspas 74).

Post a Comment

أحدث أقدم