Ni
wakati wa hisia tofauti kwa watu wa Marekani ambapo kwa kumbukumbu hii
wapo ambao wanaumizwa kwa kupoteza ndugu, jamaa na rafiki zao waliofikia
2,700 kutokana na shambulio la kigaidi lililotokea Septemba 11, 2001
katika majengo pacha ya World Trade Centre, (WTC) New York.
Eneo lililopatwa na mkasa huo leo linatengeneza tena historia
nyingine tofauti ambapo yamejengwa majengo mengine pacha yenye ghorofa
104 kila moja, huku urefu wake ni futi 1776, na thamani ya majengo hayo
ni kiasi cha Dola bilioni 3.9.

Majengo
hayo kwa sasa yanaitwa One World Trade Centre, imeripoti kuwa majengo
hayo kwa sasa huenda yakawa ndiyo majengo marefu zaidi Marekani.
إرسال تعليق