Tangu
Sitti Mtemvu atangazwe mshindi pale Mlimani City kumekua na malalamiko
kutoka kwa baadhi ya Watanzania yalifuatia kutokana na umri wake,pamoja
na taarifa nyingine ambazo yeye alizikanusha na kusema ni uzushi ikiwemo
ya kuwa na mtoto.
Baada
ya haya yote Novemba 8, 2014 Kamati ya Miss Tanzania imekutana na
waandishi wa habari Dar es salaam na kutangaza kwamba Sitti Mtemvu
ameandika barua kwa hiari yake yeye mwenyewe, kwamba amelivua taji hilo ,
hivyo kamati hiyo ikamtangaza ambaye atashikilia taji hilo kwamba ni
mshindi namba mbili wa Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima
إرسال تعليق