| Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania Mussa Leonard Mdee akizungumza na wanahabari muda mfupi uliopita jijini Dar es salaam mapema leo |
Na Karoli Vinsent
SERIKALI imepewa siku saba kuhakikisha wanafunzi wa elimu ya
Juu waliokosa mikopo kwa mwaka huu wanashughulikiwa na kupewa
mikopo,kinyume na hapo wanafunzi wametangaza kutumia njia nyingine kali
ikiwezekana kuandamana na kufanya Migomo ili kushinikiza nusu ya
wanafunzi masikini waliokosa mikopo wanapewa ili waweze kuendelea na
masomo ya elimu ya Juu.
Akitangaza Uamuzi huo mkali Leo Jijini Dar es Salaam wakati
wa Mkutano na Waandishi wa habari,Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi wa
Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania Mussa Leonard Mdee ambapo amesema
wamefikia maamuzi hayo kutokana na kushangazwa na kitendo cha Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Juu kuwanyima mikopo wanafunzi 28037 kati ya 58307
waliomba mikopo katika mwaka wa Masomo 2014-2015.
“Hali hii ni mbaya sana miongoni mwa wanafunzi waliotarajiwa
kujiunga na Elimu ya Juu,ambapo mpaka sasa zaidi ya wanafunzi
28,037wameshindwa kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo kutoka bodi
ya mikopo nchini,ingawa wanafunzi wamefaulu kujiunga na Elimu ya juu
na wanavigezo vyote vyenye kukidhi ya kupata mikopo huku ukizingatia
wanafunzi hawa ni yatima hawana Baba wala Mama harafu leo hawajapewa
mkopo”alisema Mdee.
| Edward maclein mmoja wa wanafunzi aliokosa mikopo hiyo akitoa malalamiko mbele ya wanahabari jijini Dar es salaam leo |
Mdee alizidi kusema Jumuiya hiyo hajarizika na Majibu aliyoyatoa Waziri
mkuu Mizengo Pinda Bungeni alipokuwa anajibu Swali aliloulizwa na
Mbunge wa kigoma Kusini Zitto Kabwe aliyetaka kura za Maoni za
kupitishwa katiba iliyopendekezwa isitishwe na Fedha ambazo zimetengwa
kwa ajiri ya kazi hiyo,zipelekwe kwa wanafunzi waliokosa mikopo,ambapo
waziri huyo mkuu alisema hawawezi kuhairisha kura ya maoni na kusema
madai ya wanafunzi waliokosa mikopo wanashughulikiwa na wizara ya Fedha.
“Hii kauli ya waziri mkuu inatushangaza sana kwani kujisajili
kwa wanafunzi hawa wa mwaka wa kwaza kulikoma tangu mwezi octoba
katikati na sasa ni mwezi novemba,akitambua watoto hawa masikini mpaka
sasa wako mitaani wakiwa hawajui hatma yao ,harafu anatoa majibu
yasiyokuwa na muda wa utekelezaji yaani majibu haya ni ya
kisiasa”aliongeza Mdee
Aidha, mdee alisema TAHLISO kwa kuonyesha inawajali wanafunzi
basi inatoa siku saba kamili kwa serikali kutoa fedha hizo kwa wanafunzi
waliokosa mikopo na wawe chuoni na kusema kuwa wanafunzi hawa
wamechelewa kidogo masomo kwani yameanza tangu octoba,2014 na wakaitaka
serikali kutoa mwongozo wa wanafunzi na kupolekewa vyuoni hata kama
watakuwa wamechelewa vyuoni kwa waraka maalum.
Vilevile TAHLISO waliongeza kuwa siku saba zikiisha bila
utekelezaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu kupewa mkopo,wataomba
uungwaji mkono na Asasi za Kiraia,Mashirika na haki za binadamu,wazazi
na walezi na watanzania wote mpaka wakulima kuandaa kuchukua maamuzi
magumu ili kushinikiza wanafunzi waliokuwa mitaani ambao wameshindwa
kwenda chuo kikuu kutokana na kukosa mikopo wapewe fedha hizo.
Kwa upande Edward Maclean ambaye ni mwanafunzi yatima
alinyimwa fedha na serikali,alisema anashindwa kuelewa hatma yake ya
masomo huku akizingatia hana baba wala mama.
“Kusema kweli mimi ni yatima sina baba wala mama,nimesoma
kwenye shule za kata mpaka namaliza kidato cha sita,leo nimechaguliwa
chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) naambiwa sina mkopo kutokana na
serikali kutokuwa na fedha,sijui mimi niende wapi”alihoji Maclean huku
akitokwa na machozi
إرسال تعليق