Wanafunzi
wa chuo kikuu cha Dar es salaam kutoka chama cha democrasia na
maendeleo CHADEMA leo wameibuka na sentensi tano juu ya sakata la vurugu
zilizoibuka wiki iliyopita wakati wa mdahalo uliokuwa unaendeshwa na
taasisi ya mwalimu nyerere katika ukubi wa ubungo plaza ambapo kuliibuka
vurugu kubwa na kufanya mdahalo huo kuvunjika.
Akilaani
vurugu hizo mbele ya wanahabari leo jiini dar es salaam mwenyekiti wa
CHASO Bwana JAMES MWANINYELA amesema kuna mambo matano ambayo wao kama
wanafunzi wasomi wa Tanzania wanajiuliza uhusiana na vurugu hizo,mambo
hayo ni kama yafuatayo---
1-Kwanza tunalaani vikali vurugu hizo
2-CHASO
tunahoji ukimya wa menyekiti wa CCM TAIFA ndugu JAKAYA KIKWETE kwa
baadhi ya viongozi wake na makada wa chama chake kwa kutishia kwa
kutishia usalama wa viongozi wenye heshima kubwa nchini Tanzaniayani
kama makamu wa rais mstaafu,na waziri mku mstaafu,jaji mkuu
mstaafu,anahujumiwa na mwenyekiti taifa anakaa kimya je raia wa kawaida
itakuaje?nani yuko nyuma ya makonda?
3-Kwa
kuwa Paul makonda ni katibu wa chipukizi wa UVCCM TAIFAjambo ambalo
kimsingi ndio mtendaji mkuu CHASO UDSM tunataka kujua kama huo ndio
utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya chama chake-CCM katika kulinda maoni
hatamu ya katiba pendekezwa.
4-CHASO
UDSM tunamtaka Paul makonda na baadhi ya UVCCM UDSM walioshiriki katika
vurugu hizo wajitokeze hadharani na kuomba radhi kwa aibu kubwa
waliolitia taifa.
5-Tunaomba
watanzania kushiriki kikamilifu katika chaguzi za serikali za mitaana
kukikataa Chama cha mapinduzi kwani sera zake zimeshindwa kuondoa maadui
watatu yani ujinga,maradhi na umaskini na badala yake kimeongeza adui
mwingine ufisadi.
Hizo ndio sentensi tano ambazo nimeona nikuwekee hapa mdau wangu
| Mwenyekiti wa CHASO UDSM bwana JAMES MWANINYELA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam muda mfupi uliopita |
إرسال تعليق