NISHER ni kati ya watengenezaji bora wa video Bongo ambao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko katika sekta hiyo. Jamaa huyu makazi yake yapo Arusha na kazi zake zote anafanyia huko. Kama ukiangalia video ya Jikubali iliyoimbwa na Ben Pol kisha Mama Yeyoo ya G.Nako ama video ya Nje ya Box au Chuna Buzi ya Shilole utatambua uwezo wake wa kuzipika video kiufundi.(P.T)

Mkali wa kutengeneza video Bongo, 'Nisher'.
Juzikati
Nisher alitinga ndani ya Global Publishers na kufanyiwa mahojiano katika
Kipindi cha Mtu Kati kinachorushwa kupitia Mtandao wa Global TV Online
na katika makala haya anafunguka zaidi: Unazungumziaje wasanii kurekodi
video nje ya nchi? Ni sawa kwani ni biashara na ni fedha ya mtu na
huwezi kumkataza mtu anapotaka kuwekeza.
Lakini
kwa sanaa ya nchi yetu inatakiwa uangalie unatangaza vipi nchi yako.
Muunganiko ni muhimu lakini usifanye muunganiko utakaokufanya ukawasahau
madairekta wa nchi yako. Ni kweli tatizo ni mandhari ndiyo maana
wanakimbia Bongo? Hapana! Ujue mandhari hapa Bongo zipo tena nyingi
kwangu mie wanavyokimbilia huko naona ni changamoto tena nzuri kwani
inatufanya tuone wapi tunakosea.

'Nisher' akipozi.
Ila
tatizo la Wabongo wakishafanya video huko nje watakuja na kujisifu kuwa
wamefanya kwa mkwanja mrefu lakini mtu huyohuyo akija kwako analia-lia
anataka umtengenezee hata kwa bure.
Kwa nini
gharama zako ni kubwa kurekodi? Ni kweli gharama zangu ni kubwa na
zimelenga kwa wale wenye kipato kikubwa kutokana na uzuri ninaoufanya.
Nimekuwa na uzoefu kwa kufanya kazi na wasanii wakubwa kwanza naona
inanipa wakati mzuri wa kujifunza mengi kupitia wao, namuamini na Mungu
pia.
Upoje
uhusiano wako na Weusi? Weusi ni kama familia yangu, Joh Makini ni baba,
G.Nako ni kaka na Niki wa Pili ni ndugu wa karibu. Najivunia kuwa nao
kwa sababu ni wa kwanza kunitangaza na watu wakajua kuwa kuna mtu
anaitwa Nisher.
Watu gani
wamesaidia mafanikio yako? Namshukuru Mungu kwani ndiye anayenisaidia
kufanya ubunifu pia wazazi wangu na ndugu na marafiki mbalimbali. Kwa
nini ni ngumu staa kumkubali staa mwenzake?
Wanakubaliana
ila sema kwenye nyanja za kazi hutakiwi kumpigia mwenzako magoti kwa
sababu ni kazi. Ni sawa na mabondia kabla hawajaanza mpambano
wanakumbatia lakini baada ya hapo wanaachana. Ni kweli unatoka na Lulu?
Hapana! Lulu ni rafiki yangu tu wa kawaida tena urafiki wetu ni wa ndani
ya Mtandao wa Instagram.
Yeye yupo
na maisha yake na mimi ya kwangu na mara zote tumekuwa tukitaniana sana
wala sijawahi kutoka naye kimapenzi. Kitu gani kinasababisha maprodyuza
kupotea ghafla? Kikubwa ni kulewa sifa ama kujisahau kwani ni kitu
rahisi sana,hata mie nilipokuwa naanza nilikuwa nikipata simu nyingi
huku wengi wakinipongeza na kuniambia nisilewe sifa.
إرسال تعليق