Bunge lilishambuliwa kwa gesi ya kutoa machozi kuzuia mjadala muhimu kuendelea
Polisi
katika mji mkuu wa Lagos, Nigeria, wamefyatua gesi ya kutoa machozi
ndani ya jengo la bunge, na kulazimisha kuahirishwa kwa mjadala muhimu
wa bunge hilo kuhusu kurefushwa kwa kipindi cha hali ya tahadhari
kaskazini mwa nchi hiyo.
Mwaandishi wa BBC amesema kuwa maafisa wa
Polisi walikuwa wakijaribu kumzuia spika wa Bunge la waakilishi Aminu
Tambuwal, ambaye alihamia chama cha upinzani mwezi uliopita kuendelea na
mjadala huo.
Wabunge wa upinzani wanasema kuwa hali ya tahadhari imeshindwa kuhimili visa vya wapiganaji wa kiislam wa Boko Haram.
Mwaandishi
w BBC aidha anaongeza kuwa afisa mkuu wa polisi ametakiwa kufika mbele
ya baraza la Senate kuelezea hatua hiyo ya maofisa wa polisi kurusha
vitoa machozi ndani ya Bunge.
Bunge limefungwa hadi juma lijalo.
- BBC
إرسال تعليق