Maambukizi ya Ukimwi kwa madada poa yaongezeka


Maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa wanawake wanaojiuza miili yao Zanzibar maarufu kama madada poa, yameongezeka kutoka asilimia 10 hadi asilimia 19 hali ambayo inaonyesha kuwa Ukimwi bado ni tishio.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Fereji, alisema kiwango cha maambukizi ya ukimwi Zanzibar kimefikia asilimia moja kutoka asilimia 0.6.

Alisema maambukizi hayo yapo juu zaidi hasa katika makundi maalum likiwamo la wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na kuwa maambukizi hayo kwa mwaka 2007 yalikuwa asilimia 12 hadi kufikia asilimia 2.6 mwaka 2012.

Alisema kwa upande wa vijana wanaotumia dawa za kulevya, maambukizi ya VVU yalikuwa asilimia 16 hadi asilimia 11.3. Alisema maambukizi hayo yanaongezeka kutokana na Zanzibar imezungukwa na mazingira hatarishi na kuwa mabadiliko ya haraka ya tabia za wanajamii yanahitajika ili kufanya maamuzi sahihi ndani ya jamii katika kukabiliana na maambukizi mapya.

“Lazima tufahamu kwamba kuwanyanyapaa watu walio katika makundi maalum sio tu kuwanyima hazi yao ya msingi ya kupata huduma mbalimbali za kiafya, bali ni kikwazo katika kudhibiti maambukizi ya Ukimwi ndani ya jamii yetu,” alisema Fereji.
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

أحدث أقدم