MAKOCHA WACHAGUA VIJANA KUSHIRIKI MICHUANO YA TAIFA U-12

Mwamuzi akiwakagua wachezaji.
Kikosi cha timu ya Villa Kids kikiwa katika pozi.
Mchezaji wa Bom Bom (mwenye njano) akipambana na wachezaji wa New Team (wenye nyekundu).
MAKOCHA wa Timu za Vijana chini ya umri wa miaka 15, za Kinondoni, Ilala na Temeke leo kwenye Uwanja wa Karume, Dar, wameendesha zoezi la kuchagua wachezaji watakaounda vikosi vyao vitakavyokwenda kushiriki michuano ya Taifa ya vijana wenye umri huo, yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu katikati ya mwezi Desemba jijini Mwanza.
Zoezi hilo ambalo lilianza wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Shule ya Benjamini Mkapa linatarajiwa kukamilika kesho (Jumapili) kwenye uwanja huo wa Karume ambapo makocha hao watachagua wachezaji 14 kuunda vikosi hivyo.
Wachezaji walioshiriki zoezi hilo ni kutoka kwenye timu za Villa Kids, Karume, Twalipo, Wakati Ujao, Mchanganyiko, Bom Bom, Champion, Kazad, Las Simba, EFCA, Amana Shootimg, Temeke Youth pamoja na Mbagala Youth.
(Habari/Picha: Mohamed Mdose/GPL)

Post a Comment

أحدث أقدم