
Dodoma. Makundi ya urais ndani ya CCM ni miongoni mwa mambo ambayo yameuteka mjadala wa Akaunti ya Escrow katika Bunge.
Tangu kuanza kwa mjadala wa Akaunti ya Escrow
Jumatano iliyopita kumekuwa na sintofahamu iliyotokana na baadhi ya
wabunge wa CCM kujikita katika kuangalia urais zaidi.
Hali hiyo ilifanya kupunguza ushiriki mzuri wa
baadhi ya wabunge kuhofia kuingizwa kwenye chuki ya makundi ya urais
kupitia mjadala huo.
Baadhi yao walisikika wakishutumu hatua ya
uchotaji wa fedha hizo, kiasi cha Sh321 bilioni katika makundi madogo
madogo nje ya Ukumbi wa Bunge, lakini hawakuonekana wakichangia ndani ya
Bunge.
Hata hivyo, hatua ya vyama kupewa jukumu la
kupeleka majina ya wachangiaji katika ofisi ya Katibu wa Bunge, nayo
inaonekana kuwanyima fursa baadhi ya wabunge kuchangia katika mjadala
huo.
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimroad Mkono ni
mmoja wa waathirika wa utaratibu huo, ambapo alilalamika bungeni kuhusu
kutopewa nafasi ya kuchangia.
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu alimwambia
aende kwenye chama chake akazungumze nao maana wao ndiyo walioleta
majina ya wachangiaji.
“Mimi niliomba kuchangia, lakini nikapewa masharti
kama ninataka kuipata nafasi hii niwasaidie (Serikali),” alisema mbunge
mwingine wa CCM ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Makundi ya urais
Shinikizo la kutaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kujiuzulu katika nafasi hiyo linatajwa kuwa ni miongoni mwa mambo
yanayotajwa kuwa ni mbinu za kumchafua ili mbio zake za kusaka urais
ziingie dosari.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Uhusiano na
Uratibu), Stephen Wassira alisema kama kuna watu ambao wanataka urais
kwa kuchafuana, hawafai kushika nafasi hiyo.
Mbinu hizo chafu zinatajwa kufanywa na wabunge
walio ndani ya chama chake ambao wanatajwa kuyaunga mkono makundi
mengine.Hofu hizi za makundi ya urais, yameufanya mdahalo huo kwa upande
wa CCM kujikita katika kuhakikisha kuwa kila mmoja anajilinda ili
asilichafue kundi alilomo.
- Mwananchi
- Mwananchi
Post a Comment