Na Saidi Mkabakuli, Kyela
Kutokana
na adha ya usafiri wa majini inayowakabili wakazi waishio katika fukwe
za Ziwa Nyasa, Mamlaka ya Bandari Tanzania kupitia kituo chake cha Kyela
ipo mbioni kujenga meli ya abiria na mizigo ili kuwahudumia wakazi hao.
Hayo
yaliwekwa bayana na Mkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema
wakati timu wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya
Mipango ilipotembelea na kukagua bandari za Itungi na Kiwira zilizopo
wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.
Bw.
Ntetema alisema kuwa Mamlaka imeshakamilisha mchakato wa manunuzi na
tayari imempata mkandarasi M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya
ujenzi wa meli yenye uwezo wa kubeba jumla ya tani 200 za mizigo na
abiria 200.
“Mamlaka
ipo kwenye hatua za mwisho za kuandaa mkataba unaotarajiwa kutiwa saini
mwezi ujao na kazi itaanza mwanzoni mwa mwaka ujao,” alisema.
Bw. Ntetema
Aliongeza
kuwa mpaka sasa Bandari ya Kyela imeshaanza maandalizi ya kuvuta umeme
uliofadhiliwa na Wakala wa Umeme Vijijini pamoja na kuaanza kwa kujenga
matishari mawili ili yaweze kurahisisha utoaji wa huduma mara meli hiyo
itakapoanza kazi mwishoni mwa mwaka ujao.
Kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri aliupongeza uongozi wa Mamlaka
kwa hatua yake hiyo kwani itaongeza tija ya shughuli za kiuchumi katika
kanda hiyo ya Ziwa Nyasa.
“Ninaupongeza
uongozi wa Mamlaka ya Bandari kwa kuanza mchakato huu utakaofungulia
fursa za kiuchumi na maendeleo kwenye ukanda huu, hivyo kuunga mkono
jitihada za serikali za kupunguza vikwazo mbalimbali vinavorudisha kasi
ya kusaka kupunguza umaskini nchini,” alisema.
Bibi
Mwanri aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutatoa fursa za
kuhudumia shehena na abiria kutoka mikoa ya Mbeya, Njombe, na Ruvuma.
Pamoja na kuhudumia nchi za jirani ikiwemo Malawi, Msumbiji na Zambia.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 –
2015/2016) bandari ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye
lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi
wa uchumi kwa watu walio wengi.
Vipaumbele
vingine ni Kilimo ambapo lengo kuu likiwa ni kuongeza tija katika
uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na
ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya viwanda: Msisitizo umewekwa
katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi
zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo, mbolea, saruji, makaa
ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini kwa lengo la
kuongeza mapato ya Serikali.
Pamoja na kipaumbele cha Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi: Mpango
unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya
ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma)
katika kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na
kijamii; na Utalii, Biashara, na huduma za Fedha ambapo jitihada
zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa kuuza katika masoko ya ndani na
nje, kuongeza idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na
kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema akiwakaribishia wakaguzi wa
timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango ilipofika ofisini kwake.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema akifafanua jambo kwa Timu ya
ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kiongozi wa timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence (kulia) akihoji masuala mbalimbali yanayohusiana
na shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na Bandari ya Kyela.
Kiongozi wa timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence (kulia) akihoji masuala mbalimbali yanayohusiana
na shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na Bandari ya Kyela.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema akifafanua jambo kwa Timu ya
ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema akifafanua jambo kwa Timu ya
ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kiongozi wa timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence (Mbele) akiwaongoza wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa
miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kupanda boti
ili kwenda kushuhudia lango la kuingilia Gati la Bandari ndogo ya
Itungi. Itungi ni bandari ya kipekee nchini kujengwa mtoni.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema (Kulia) akiwaonesha kitu
wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango wakati wakishuhudia lango la kuingilia Gati la Bandari
ndogo ya Itungi.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema (Aliyevaa tai) akiwapa
maelezo wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo sehemu
inapojengwa gati mpya (halionekani) katika Bandari ya Kiwira.
Wajumbe
wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango walipata fursa ya kujionea meli pekee inayotoa huduma ya
kusafirisha abiria na mizigo (MV Songea) katika Ziwa Nyasa kwa upande wa
Tanzania.
Wajumbe
wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango walipata fursa ya kujionea meli pekee inayotoa huduma ya
kusafirisha abiria na mizigo (MV Songea) katika Ziwa Nyasa kwa upande wa
Tanzania.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema (Aliyevaa tai) akiwaambia
jambo wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo sehemu
inapojengwa gati mpya (halionekani) katika Bandari ya Kiwira.PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI
إرسال تعليق