
Bunge lilifikia uamuzi huo mjini Dodoma juzi baada
ya mvutano mkali kati ya wabunge na Serikali kuhusu utekelezaji wa
mapendekezo ya PAC.
Katika kupitia mapendekezo ya PAC, Serikali
ilileta hoja ya kubadilisha mapendekezo ya kamati hiyo ambayo
yalijadiliwa ndani ya Bunge. Bunge liliazimia vyombo vinavyohusika na
uchunguzi kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow kuendelea na
uchunguzi na vile ambavyo havijaanza vifanye hivyo ili kubaini ukweli na
kuchukua hatua kwa watu wote waliohusika.
Pia, Bunge liliazimia kuzitaka mamlaka
zinazohusika ikiwamo Benki Kuu kuchukua hatua dhidi ya benki zote
zilizohusika na miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Azimio jingine ni kuitaka Serikali ifanye mapitio
yote ya mikataba ya umeme na kutoa taarifa bungeni kabla ya kikao
kinachofuata cha Bunge kuhusu utekelezaji wake mapema kabla ya Bunge la
Bajeti la mwaka 2015/2016.
Kuhusu kuiwajibisha bodi ya Shirika la Umeme
nchini, (Tanesco), Bunge liliishauri Serikali ifanye uchunguzi na
kuwachukulia hatua wote waliohusika na kashfa hiyo.
Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Eliakim Maswi kuwajibika kutokana na sakata hilo, Bunge limeazimia
kulifikisha suala hilo kwa mamlaka ya uteuzi kwa hatua zaidi.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق