MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari juzi aliongoza wapiga kura wake kugawa shamba linalomilikiwa na Chama cha Ushirika mkoani Arusha (ACU), akisema amechoka kuona wananchi wake wakisotea ardhi ilhali kuna maeneo hayaendelezwi.
Nassari
aliongozana na wapiga kura wake hadi eneo la shamba la Valeska na
kuanza kuwagawia ardhi bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mmiliki wa
ardhi husika.
Akiwa katika eneo hilo, alipima ardhi kwa kuhesabu hatua na kuigawa kwa wapigakura wake wenye uhitaji wa ardhi.
Kutokana
na uamuzi wake huo wa kujichukulia madaraka na kuigawa ardhi kuonekana
kuwashangaza wengi, mwandishi wa habari hizi alilazimika kuomba
ufafanuzi wa tukio hilo kupitia simu yake ya kiganjani, ambapo alisema
amelazimika kuchukua uamuzi huo anaouona unafaa ili wananchi wake wapate
ardhi.
Alisema
amelazimika kuingilia kati suala hilo, kutokana na migogoro isiyoisha
ya ardhi wilayani Arumeru kwani awali wahusika wa ushirika huo walitoa
ekari 1,500 za ardhi na kuzigawa kwa wananchi ili kuepusha maandamano na
uvamizi wa mara kwa mara, lakini kinyume chake ardhi hiyo hawakupewa
wananchi, bali madiwani wa Halmashauri ya Arumeru wamekuwa nao wakiitaka
ardhi hiyo.
Aidha,
alisema wakati wananchi ambao ni wapigakura wake wakidai ekari hizo,
kuna watumishi wamejitwalia ekari 400 kati ya hizo 1,500 zilizotolewa na
ACU na kujimilikisha wao huku watumishi hao bila kuwataja majina
wakiwakodishia wananchi wake.
Alisema
madiwani wa Halmashauri hiyo walitoa ekari 500 na kuwapa wananchi na
ekari nyingine wakipanga mambo yao na kutokana na hali hiyo, anaamini
kuna maslahi ya watumishi wa halmashauri hiyo.
“Kutokana
na hali hiyo nimeamua kama mbunge nigawe ardhi mwenyewe kwa kupima kwa
miguu ili kila mwananchi aweze kupata ardhi sababu watendaji wameshindwa
kusimamia haki.
“Hapa
ndio nimeanza na nitaendelea kugawa ardhi kwenye mashamba
yasiyoendelezwa na hayo ndio maamuzi yangu kama Mbunge. “Nasema siwezi
kukubali wananchi wangu kila siku walalamikie masuala ya ardhi wakati
kuna madiwani, Mkuu wa Wilaya (DC) na viongozi mbalimbali. Nimegawa
Valeska, bado nitakweenda Mbughuni hadi Kikuletwa nitagawa ardhi, kama
Mbunge nimechoka na migogoro isiyoisha”.
Suala
la Nassari kugawa ardhi bila kufuata utaratibu liliibuka mara baada ya
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George
Simbachawene kufanya kikao na maofisa ardhi na wapimaji wa Mkoa wa
Arusha kutoka Halmashauri tatu za Jiji la Arusha, Arusha Vijijini na
Arumeru ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo na kutafuta suluhu ya migogoro
hiyo.
Katika
mazungumzo hayo na watumishi hao, pia walifika viongozi kutoka ACU
ambao walisema chama hicho kilishatoa ekari 1,500 kwa wananchi wa wilaya
hiyo, lakini madiwani walikataa eneo la Mashariki walilopewa na kutaka
wachague eneo wanalolitaka wao.
Alisema
ACU imeshatoa eneo hilo ili kuwapa wananchi, lakini kuna milolongo
mingi ikiwemo masuala ya siasa kati ya madiwani ambao hawakubaliani na
maamuzi ya ACU.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii, Mjumbe wa Bodi ya ACU, Furahini Mungure
alisema shamba hilo la ACU ni kubwa na linahitaji kuendelezwa ikiwemo
kujenga vitega uchumi sambamba na mradi wa ghorofa 17, hivyo kutokana na
mgogoro huo ukiwamo wa suala la Nassari kugawa ardhi kunarudisha nyuma
masuala ya uwekezaji.
“Tunamshangaa
Mbunge kwa kitendo cha kugawa ardhi tunayoimiliki bila kufuata
taratibu, yeye amechukua kinamama, watoto, wazee, vijana na kwenda
kuwagawia ardhi kwa kuwapimia na miguu… sasa hii ni siasa ili aonekane
ni mwema kwao kumbe hakufuata taratibu hivyo tunakuomba Naibu Waziri
uingilie kati mgogoro huu,” alisema.
Alisema
wakati Nassari alipokuwa akigawa ardhi hiyo, Polisi walifika eneo hilo
la shamba la Valeska ili kumwamuru mbunge huyo na wananchi wasitishe
kugawana ardhi, lakini bila ya kutumia nguvu.
“Polisi
walimhoji Nassari kwa nini anafanya hivyo, lakini yeye aliendelea
kugawa ardhi na hapo tunawapongeza polisi licha ya ardhi ya shamba letu
kugawiwa na mbunge kwa wananchi sababu kulikuwa na wananchi wa rika
mbalimbali wakiwemo watoto kama wangeweza kuchukua maamuzi magumu watu
wangeumia.
“Lakini
kwa busara, polisi waliondoka na kumwacha Nassari akigawa ardhi ambayo
si halali kwa wananchi, hivyo hatujui hii ni mbinu ya mtaji wa kisiasa
au ni nini maana masuala ya ugawaji ardhi yana taratibu zake kisheria,”
alisema.
Mkuu
wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Benedict
Mapujila alisema polisi walitumia busara maana kulikuwa na wananchi
wengi pamoja na watoto.
Naye
Simbachawene alisema inashangaza kuona Mbunge anayejua sheria, taratibu
na kanuni kuchukua maamuzi yasiyofaa na kuahidi kuonana naye ili
kuzungumza zaidi juu ya suala hilo.
Pia
alisema atapanga ziara ya kukutana na madiwani wa Halmashauri hiyo
pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo, Nyirembe Munasa ili kutatua mgogoro huo,
kwani ameshindwa kukutana nao kwa sasa kutokana na misiba iliyotokea
ambayo ilisababisha wafanyakazi wa halmashauri hiyo kufa kutokana na
ajali eneo la Nduruma.
Wilaya
ya Arumeru imekuwa na migogoro mingi ya ardhi hali inayosababisha
wananchi kuvamia mara kwa mara mashamba ya wawekezaji kwa madai ya kuwa
mashamba hayo hayajaendelezwa

إرسال تعليق