
Mkuu wa Wilya ya Kati
aliyepo Kati kati aliyenyanyua mkono juu Nd. Vuai Mwinyi akimpatia
maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kuhusu ujeni wa
jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Kati liliopo Dunga.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Mjumbe wa Kamati Kuu
ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema Chama
cha Mapinduzi kitaendelea kushinda uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka kesho ili
Serikali inayoongozwa na Rais wa Sasa wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Shein
imalize kipindi chake cha Pili.
Balozi Seif alisema
hayo katika Mkutano wa hadhara wa Wanachama wa CCM Jimbo la Koani
uliofanyika Kiwilaya hapo kwenye uwanja wa michezo wa Unguja Ukuu baada
ya kutembelea ujenzi wa Ofisi za CCM Wadi na Matawi zilizomo ndani ya
Wilaya ya Kati.
Alisema ushindi huo
utapatikana na kuuzika kabisa upinzani usio na sera endapo wanachama wa
chma cha Mapinduzi pamoja na Wananchi wote watapiga kura kwa kuendelea
kuiunga Mkono CCM.
Balozi Seif alieleza
kwamba mwaka 2015 ni kipindi muwafaka kwa chama cha Mapinduzi kuuzika
upinzani unaoonekana kushindwa kuongoza dola tokea kuanzi kwa mfumo wa
vyama vingi vya siasa nchini Tanzania mapema katika miaka ya 90.
Alionyesha kuchukizwa
kwake na tabia ya viongozi wa upinzani ya kujaribu kuupotosha umma kwa
kumwita msaliti wa kuuza ardhi ya Zanzibar huko Tanzania Bara.
Balozi Seif alisema
kitendo hicho cha udhalilishaji kinaonyesha dharau kubwa anayofanyiwa
ambayo kwa sasa inastahiki kujibiwa kwa nguvu zote zinazostahiki dhidi
ya wapinzani hao.
Akitoa ufafanuzi
kwenye mkutano huo kuhusu suala la ardhi linavyopotoshwa na wapinzani
ambalo wanalinakili kimakosa kupitia katiba iliyopendekezwa na bunge
Maalum la Katiba Mjumbe wa Bunge hilo ambae pia ni Waziri wa Ardhi,
Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban alisema hakuna
kipengele kichoelezea ardhi ya Zanzibar kuhodhiwa na Muungano.
Mh. Shaaban alisema
kilichomo ndani ya Katiba inayopendekezwa ni kumpya haki na fursa kila
Mtanzania awe anatoka Zanzibar au Tanzania Bara kumiliki ardhi katika
sehemu ya Jamuhuri ya Muungano endapo katiba hiyo itapita.
Alisema katika mfumo
uliowekwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na haki ya kupanga
au kusimamia matumizi ya ardhi yote iliyomo ndani ya Visiwa vya Zanzibar
wakati ile ya Bara itasimamiwa na Serikali ya Muungano mfumo ambao
utampa haki Mtanzania ye yote kutumia ardhi hiyo.
Mapema Balozi Seif
alikaguwa ujenzi wa Ofisi ya CCM Wadi ya Jumbi, Maskani ya CCM ya Mwera
Pongwe, Tawi la CCM Mchangani, Tawi la CCM Bambi ya Bondeni pamoja na
Tawi la CCM Kijundu.
Akiahidi kusaidia
uwezekaji paa wa Tawi la CCM Kijundu na mifuko ya saruji kwa Tawi la CCM
Mchangani Balozi Seif alisisitiza umuhimu wa wanachama hao wa CCM
Matawi na wadi mbali mbali Nchini kusimamia uanzishwaji wa miradi ya
kiuchumi katika Ofisi mpya wanazojenga.
Balozi Seif alisema
mfumo wa Chama umeelekeza kwamba ofisi za Chama zinazojengwa kuanzia
Maskani hadi mikoa lazima ziwe na miradi ya kiuchumi mpango ambao
uawavua wanachama kuwa tegemezi kwenye miradi yao.
Aliwakumbusha wana CCM
hao kujiandaa vyema na kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika mwishoni
mwa mwezi aprili mwakani pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao.
Alisema kazi ya
ushindi wa Chama cha Mapinduzi itakuwa rahisi kutokana na umadhubuti wa
chama chenyewe utaosimamiwa na wanachama na viuongozi wao.
Alieleza kwamba wakati
CCM inamaliza kutekeleza ilani na sera zake kwa ufanisi mkubwa
ulioshuhuidiwa na kila mtu, hivi sasa inajiandaa kutengeneza ilani
nyengine mpya kwa ajili ya kuinadi wakati wa kampeni za uchaguzi za
mwaka ujao.
إرسال تعليق