MDADA WA KICHINA AWAPIKU WADADA WA KIBONGO KWA KUKATA NYONGA


Kama kawa ni siku nyingine ambayo Mapaparazi Wetu, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ anayewakilisha Mji Kasoro Bahari, Richard Bukos ‘Mpigapicha Mkuu,’ Musa Mateja ‘Toz’ na Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’ walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kuwasiliana moja kwa moja na mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili yaliyopo Bamaga Mwenge jijini Dar es  Salaam.
Saa 3:53 usiku
MDADA WA KICHINA AWAPIKU WADADA WA KIBONGO KWA KUKATA NYONGA
Mkuu akiwa ofisini anaangalia saa yake na kubaini kuwa inakaribia kabisa kutimia saa nne usiku hivyo anaamua kumpigia Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’ aliyekuwa ndani ya kiwanja cha Club East 24 Mikocheni jijini Dar.
Mnally: Haloo Mkuu wangu nakupata.
Makao Makuu: Najua kama unanipata, nataka kujua uko wapi na nini kinaendelea hapo ulipo?
Mnally: Mkuu kama kawa niko katika kiwanja cha kijanja cha Club East 24 hapa Mikocheni kwenye onesho la B Band.
Makao Makuu: Vipi mpaka muda huu umeshabamba vituko gani?
Mnally: Mkuu si unajua hii bendi licha ya kuwa na vibao vyake pia inapiga kopi za nyimbo maarufu ulimwenguni, sasa muda si mrefu lilikuwa likirindima sebene la Kisanola lililopigwa na Koffie Olomide, Banana ndiye alikuwa akijifanya Koffie yaani Mkuu ilikuwa fulu vituko kutokana na wadada wa Kichina kuvamia jukwaa na kuonesha ufundi wao wa kukata nyonga.
Makao Makuu: Du! Wachina si hawajabarikiwa sana mambo flani ya kufungashia wowowo?
Mnally: Mkuu hao ni Wachina wa zamani, hivi sasa hakuna Mchina wala Mhindi wote wanakimbizana na Wabongo.
Makao Makuu: Enhe, nipe kinachojiri maana nasikia makelele kwa sana.
Mnally: Mkuu kufuatia Banana kukonga nyoyo za watu kwa miondoko ya Kisanola, mashabiki wamemuomba arudie, kuna wadada watatu wa Kibongo walikuwa wanashindana ndipo ghafla steji ikavamiwa na  dada wa Kichina, anakata nyonga balaa yaani kawafunika wote ndiyo mashabiki wanamshangilia.
Mkuu halafu kabla hatujaagana Banana wakati akiimba ‘waini’ yake aliificha sehemu sasa naona kuna dada mmoja ameikwapua lazima nimuoneshe.
Makao Makuu: Sawa Mnally, lakini mbona leo umeripoti bila kigugumizi! Haya kijana piga kazi mimi ngoja nimcheki Musa Mateja ‘Toz’.
Saa 6:43 usiku
MKE WA FERGUSON WA MASHUJAA MUSICA AZULIWA KAUMBEYA
Makao Makuu: Haya Musa Mateja niambie kijana wangu uko pande zipi?
Mateja: Mkuu niko Kijitonyama ndani ya Ukumbi wa Cheetoz Miti Mirefu, Bendi ya Mashujaa Musica inakamua.
Makao Makuu: Vipi pana matukio gani hapo ya kuwahabarisha wasomaji wetu?
Mateja: Mkuu hapa burudani zinaendelea kama kawa jukwaani muda huu anarap huyu rapa wao, Saulo John ‘Ferguson’ huku mkewe, Angel Bushoke akimuwekea ulinzi kwa pembeni.
Makao Makuu: Dah huyo mwanamke kazidisha wivu, yaani kila anapokwenda mumewe naye yupo nyuma yake, ndiyo maana wenzake wanamsengenya kwamba tabia hiyo inasababisha kupata ‘kitumbo’ mara kwa mara.
Mateja: Mkuu, huo umbeya hata miye nishausikia kama mara tano hivi.
Makao Makuu: Sawa Mateja piga kazi ngoja nimcheki Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos sijui yuko kiwanja gani.
MVUA YATIBUA ONESHO LA KUMWAGA RADHI
Saa 7:12 usiku
Makao Makuu: Haloo, halooo Bukos haraka niambie uko wapi na nini kinaendelea?
Bukos: Mkuu niko maeneo ya Mburahati Madoto kuna nyumba moja kesho wana Send Off lakini leo kuna mkesha wa kigodoro sasa watu wamefurika na kuna kundi la wadada wa Magomeni Kagera wamekuja hapa wanataka kumwaga radhi.
Makao Makuu: Sasa imekuwaje?
Bukos: Mkuu hivi tunavyozungumza mvua imeanza kunyesha kwa kasi na muziki wenyewe umefunikwa, naona watu wanatawanyika, nami sitakaa sana maana hali ya hewa imeshavurugika.
Makao Makuu: Hiyo mvua kama siyo ya mgawo nahisi itakuwa inanyesha mji mzima, maana hata huku Sinza inamwagika, poa Bukos piga kazi ngoja nimcheki Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ anipe ripoti ya Mji Kasoro Bahari.  
Saa 8:23 usiku
Makao Makuu: Haya Mkude Simba, hebu nipe ripoti ya kinachojiri hapo ulipo.
Shekidele: Mweeh, Mkuu niko ndani ya kiwanja kipya kinaitwa Kilimanjaro, Nani Mtani Jembe, kipo hapa karibu na Tanesco Makao Makuu.
Makao Makuu: Kuna nini hapo?
Shekidele: Mkuu hapa kuna uzinduzi wa bendi mpya inaitwa Salena iko chini ya mkongwe wa dansi, Bashiri Uwadi, yaani kuna nyomi la watu, hivi tunavyozungumza namuona Mkurugenzi wa huu ukumbi, Suzy Mizani naye amekuwa baamedi anahaha kuhudumia vinywaji wateja.
Makao Makuu: Vipi lakini burudani yao ikoje?
Shekidele: Mkuu hawa vijana wakijitahidi watafika mbali sana maana mashabiki wamewapokea vizuri, ukumbi mzima umejaa watu kibao wanacheza nyimbo zao utafikiri wameshazizoea. Yaani Mkuu hii bendi imezinduliwa kwa mbwembwe sana maana wanamuziki wamepiga pamba si za mchezo ukicheki ukumbi ulivyopendeza ndiyo usisema, idara ya ulinzi ipo fiti mno kwani kuna mabaunsa kibao, Mkuu hiki kiwanja nahisi kitatuongezea matukio.
Makao Makuu: Sawa Shekidele piga kazi ukitoka wapigie wenzako uwaambie mkapumzike.
Shekidele: Poa Mkuu wangu.

Post a Comment

أحدث أقدم