Kikosi cha zimamoto
Akizungumza na NIPASHE, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Jeshi hilo, Miraji Killo alisema:
“Tunapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wananchi kutokana na kutoridhishwa na huduma zetu, lakini sisi tumejipanga kumaliza changamoto zote na kutoa huduma bora kwa jamii hasa katika majanga ya moto.”
Alisema kuwa magari makubwa ya kuzimia moto yaliyopo hivi sasa hayaendani na mabadiliko ya kukua kwa miji nchini kutokana na hivi sasa maghorofa marefu yanayojengwa na Jeshi hilo hayana vifaa vya kisasa vya kuzimia moto.
“Zamani tulikuwa tukienda kwenye tukio hatuishiwi na maji kutokana na visima vyetu kuwa na maji ya kutosha tofauti na sasa, kuna shida kubwa ya maji, visima vingi vimefukiwa kutokana na ujenzi wa barabara,” alisema Killo.
Alisema Jeshi hilo limefanya mazungumzo na wenyeviti wa serikali za mitaa wote kujenga visima vya maji katika mitaa yao ili janga lolote la moto likitokea wapate huduma kwa haraka.
Zimamoto wamekuwa wakilalamikiwa na kila uchao na wananchi kutokana na kuchelewa kufika maeneo ya majanga na wakati mwingine wanapoishiwa na maji wanashindwa kupata mengine na matokeo yake ni majengo na mali nyingine kuteketea.
CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق