“Serikali hutenga fedha nyingi kila mwaka kwa
ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili vijana wanaojiunga na vyuo
vikuu wakopeshwe, sasa kwa nini inaupendeleo?” alihoji.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama alisema utoaji wa mikopo hufuata
taratibu za kisheria na miongozo ya Serikali hasa katika vipaumbele vya
Taifa.
“Mahitaji ya kitaifa ndiyo yanayoiongoza Serikali
kuainisha programu zinazopewa kipaumbele katika kutoa mikopo kwa nia ya
kuwashawishi wanafunzi wasome,” alisema.
Alisema kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015
vipaumbele vya Taifa ni Ualimu wa sayansi na Hisabati, Sayansi za Tiba,
Uhandisi wa umwagiliaji pamoja na gesi na mafuta.
“Sambamba na hilo, Serikali imeendelea kutoa
mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji wanaosoma kozi zisizo za kipaumbele
na waliokidhi viwango vinavyotakiwa katika kupata mikopo,” alisema.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق