Mshambuliaji wa zamani wa Simba Mnigeria, Emeh Izuchukwu(mwenye jezi ya bluu)
Na Wilbert Molandi
BAADA ya Kamati ya Usajili ya Simba kulipitisha jina la mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Mnigeria, Emeh Izuchukwu kwenye usajili wao, uongozi wao hivi sasa upo kwenye mipango ya kusitisha mkataba wake kwenye Klabu ya Eleverum inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Norway.

Simba ipo kwenye mipango ya usajili wakati huu wa dirisha dogo
lililofunguliwa tangu Novemba 15, mwaka huu ikiwa ni mipango ya
kuimarisha kikosi chao baada ya kuanza msimu kwa kuyumbayumba.Taarifa
kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimeeleza kuwa, tayari wameanza
mazungumzo na Eleverum kwa ajili ya kuuvunja mkataba ili arejee Simba.
Kiliongeza kuwa, Simba wanaamini mazungumzo yao na klabu hiyo
yatafikia pazuri na mshambuliaji huyo atatua kuichezea timu hiyo kwenye
usajili wa dirisha dogo kabla halijafungwa Desemba 15, mwaka huu.
“Usajili wa Izuchukwu ni mgumu katika kumpata, licha ya mwenyewe
kutaka kurejea kuitumikia timu yake ya zamani ya Simba, kwa sababu ili
asaini Simba basi ni lazima mkataba wake tuusitishe kwenye klabu yake
anayoichezea.
“Tupo kwenye mazungumzo na viongozi wa klabu anayoichezea ya Norway
kwa ajili ya kuvunja mkataba alioubakisha wa kuitumikia Eleverum, mara
tutakapomalizana haraka atatua nchini kwa ajili ya kuichezea Simba,”
kilisema chanzo hicho.
إرسال تعليق