MSANII
wa vichekesho (komedy) kutoka Nigeria,Okopcha Bright Onyekere maarufu
kama Basket Mouth amewasifu wasanii wa Tanzania kwa juhudi wanazofanya
kuelimisha jamii kutumia vipaji vyao.
Akizungumza
Dar es Salaam jana baada ya kuwasili kutoka Nigeria kwa ajili ya onesho
maalum kushirikiana na wasanii wa Tanzania juzi Dar es Salaam alisema
kutoka aanze sanaa ya vichekesho miaka 16 iliyopita amekuwa akipata sifa
za wasanii wa Tanzania wakiwika katika fani za muziki, sanaa za filamu,
michezo ya kuigiza na vichekesho.
Onyekere
aliyetamba nchini Nigeria na Bara la Afrika katika fani hiyo amekuja
kufanya onesho moja lililopangwa kufanyika jana hoteli ya Golden Tulip,
aliongeza kuwa sanaa ni utajiri mkubwa kama vipaji walivyopewa
vitatumika ipasavyo na kutawala jukwaa .
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku alisema lengo la kumleta msanii
huyo wa komedy ni kuimarisha sanaa ya vichekesho kwa wasanii chipukizi
wa Tanzania ambao wanahitaji kuandaliwa kwa soko hilo nchini na nje ya
nchi.
Alisema
Kampuni ya Vuvuzela imejitolea kusaidia wasanii wa vichekesho nchini na
kuwafundisha namna watakavyoweza kuendeleza fani hiyo kazi iliyoanza
miaka minne iliyopita kampuni ilipoanzishwa.
Bukuku
alisema kila mwisho wa mwezi kuna onesho maalum ambalo hutumika
kuonesha vipaji vya wasanii wa vichekesho na jinsi msanii anavyoweza
kutawala jukwaa kuwaburudisha watazamaji.
Alisema
kampuni yake inatarajia kufanya maonesho kama hayo mikoa mbalimbali ya
Tanzania kuibua wasanii wengine wenye uwezio katika fani hiyo.
Mkurugenzi
Bukuku alisema katika onesho la karibuni Watanzania walikongwa nyoyo
zao pale wasanii wa Tanzania washirikiana na wasanii wa vichekesho
kutoka Kenya ambaye ni Mdomo Baggy na Dick Omondi kutoka Uganda anayejulikana kama Uncle Bob kufanya onesho kali nchini.
Bukuku aliwashukuru wadhamini waliojitokeza kusaidia kufanyika kwa onesho hilo ambao ni Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA),Hoteli ya Golden Tulip, Gazeti la Mwananchi
Communications, Clouds Media Group, Ultimate security, Simu TV, Prime
Advertising, Dar insites, Advertising Dar, Bongo 5, Eventlites, Hugo Domingo na Michuzi Blog.
إرسال تعليق