Mbunge huyo alitoa kauli hiyo bungeni jana alipouliza swali la nyongeza.
“Uwatake radhi wasichana wote kwa kuwadhalilisha.
Unasema kama wenyeviti wa Serikali za Mitaa wakikataa kuwa watoto huwa
‘hawapigwi’ mimba, itawezekana kupunguza mimba za utotoni. Viongozi
wangapi kuanzia ngazi ya Taifa ambao wamechukua hatua kwa watoto
waliopata tatizo hilo?” alihoji.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia alisema suala la kuzuia mimba za
utotoni ni la watu wote.
“Ukitembea barabarani unakutana na vibinti vidogo
vinatembea saa 2.00 usiku. Maeneo mengine kuna sheria zinazokataza
watoto wadogo kuingia katika vibanda vya sinema,”alisema.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu
(CCM), Riziki Said Lulida alihoji kwamba Serikali ina mkakati gani wa
kutatua tatizo la mimba za utotoni kwa kuwa Lindi inaongoza kwa tatizo
hilo, hali inayosababisha kufanya vibaya katika sekta ya elimu.
Akijibu, Mwanri alisema Serikali imekuwa ikihamasisha jamii kufuatilia mahudhurio ya watoto wao shuleni.
Alisema imeboresha somo la elimu rika kwa kutoa elimu ya afya ya uzazi inayoendana na makuzi.
Naibu Waziri Mwari alisema watu wanaobainika
kuwakatiza masomo watoto au kuwashawishi kuingia katika mahusiano ya
kimapenzi, huchukuliwa hatua za kisheria .
“Lakini tumeandaa vipindi na programu mbalimbali
zinazohimiza uzazi salama na kuepuka mimba za utotoni kupitia radio,
machapisho, televisheni, warsha na semina,” alisema.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق