KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Bw. Abdulrahman Kinana, amesema Serikali inaweza kukitoa kafara chama
hicho kwa sababu ya kuchelewesha fedha za miradi ya maendeleo ambayo
iliahidi kuitekeleza kwa wananchi.
Bw. Kinana aliyasema hayo juzi kwenye
mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara na
kusisitiza mbunge na madiwani wa chama hicho wapo katika wakati mgumu.
Alisema Serikali iliahidi mambo mengi kwenye
Uchaguzi Mkuu 2010 lakini hadi sasa fedha zilizopelekwa kwenye
Halmashauri ya Newala mwaka 2014/15 ni asilimia 13.
Aliongeza kuwa, madiwani na Mkurugenzi wa
Halmashauri wameahidi mambo mengi kwa wananchi wakiamini watapata fedha
zilizotengwa kwenye bajeti lakini matokeo yake zimepelekwa fedha kidogo.
"Kitendo cha Serikali kushindwa kuleta fedha
za maendeleo ya wananchi kwa wakati au kutopeleka kabisa, kinawaumiza
madiwani waliotoa ahadi kwenye kampeni zao mwaka 2010...nitakwenda
kuwaleza walete fedha za miradi kwa wakati," alisema.
Bw. Kinana aliwajia juu watu wanaogawa
pembejeo za kilimo na kudai wakulima hawapelekewi kwa wakati na wakati
mwingine wanatoa pembejeo hizo kwa kujuana hivyo kukwamisha dhana nzima
ya Kilimo Kwanza.
"Pembejeo hazipelekwi kwa wakati lakini
wakati mwingine zinapelekwa kwa kujuana...hali hii inarudisha malengo ya
Serikali kuwapatia wananchi pembejeo, kuna kuna wakati zinapelwekwa
zikiwa hazifai kwa matumizi," alisema Bw. Kinana.
إرسال تعليق