Imetokea
nchini India baada ya mama mmoja kujifungua mtoto mwenye miguu minne na
mikono minne huku akipokelewa na wenyeji kwa furaha kubwa na kuitwa ‘Mungu Mvulana’
Mtoto huyo amepewa jina la ‘Mungu Mvulana‘
kwa kuwa kuzaliwa na viungo kama hivyo si jambo la kawaida na
huchukuliwa kama mfano wa Mungu kwa jamii za kihindu na watu walisafiri
kutoka kona mbalimbali za nchi hiyo kwenda kumshuhudia mtoto huyo wa
maajabu.
Katika mji wa Kaskazini mwa nchi hiyo watu walijazana nje ya eneo la
Hospitali hiyo wakiwa na hamu ya kutaka kumwona mtoto ambaye ana maana
kubwa kwa jamii za nchini humo na wenyeji wa huko wana amini ataleta
baraka katika jamii zao.
Mamia ya watu walikua wamejaza nje ya Hospitali hiyo wakiimba na
kusali lakini hawakuweza kufanikiwa kumwona kutokana na wingi wao huku
Polisi wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia.
Baadhi ya watu walidiriki kusema ujio wa mtoto uyo ni dalili za
mwisho wa dunia kutokana na jinsi baadhi ya jamii nchini humo
zinavyoamini, Watalaam wa mambo ya uzazi walisema kuzaliwa mtoto huyo
akiwa katika hali hiyo ilikua na dalili ya kuzaliwa watoto mapacha ambao
kitaalam wanaitwa Parasitic twins lakini haikuwezekana na kudai ni mipango ya Mungu.
Familia ya mtoto huyo imejawa na furaha kwa ongezeko la mwanafamilia
mwingine na wanamuona mtoto huyo kama Mungu, mtoto wa kiume wa familia
ya Wahindu,Brahma ambaye anatambulika kwa kuwa na miguu na mikono minne.
إرسال تعليق