Kuanzia
mwishoni mwa wiki iliyopita kulikua na stori imesambaa sana kwenye
mitandao ya kijamii kama instagram, facebook na twitter kuhusu msichana
wa kazi ambae alitegeshewa na Baba mwenye nyumba kamera nyumbani na
baadae video iliyorekodiwa ikamuonyesha akimpiga mtoto wa mwenye nyumba.
Baadae zilitoka stori mbalimbali kwamba Mtoto mwenyewe ambae ana umri
wa miaka miwili amefariki, ni stori ambazo ziliambatana na taarifa
nyingine zisizo na ukweli ambazo Bill The African amefatilia moja baada ya nyingine kama
ifuatavyo.
- Msichana huyu wa kazi anaitwa Tumuhairwe ana umri wa miaka 22 na sio 25 kama ilivyoripotiwa ambapo ana siku 26 tu toka aanze kufanya kazi kwenye familia ya mtoto huyo.
- Kwa sasa yuko rumande kwenye gereza la Luzira Uganda na atafunguliwa mada ya kutaka kuua.
– Unaambiwa haya yote yasingejulikana kama Polisi isingemkamata baba
mzazi wa mtoto huyu, yani baba alipoona ile video ndio akampiga
Msichana huyu wa kazi ambae baada ya kipigo alikwenda kumshitaki baba wa
mtoto Polisi.
- Polisi walipomchukua Erick Kamanzi (Baba wa mtoto) nyumbani kwa ke na kumfikisha Polisi ambako alieleza sababu za kumpiga Msichana huyu na kuwaonyesha Polisi hii video hapa chini ambayo ni ya tukio la mtoto wake kupigwa.
- Baada ya hapo Polisi ndio wakamwachia na kumkamata Msichana huyu wa kazi.
- Erick ambae ndio baba mzazi wa mtoto huyu amesema wanashukuru Mungu mtoto kuwa hai bila matatizo na sasa mtoto amekua karibu na baba yake zaidi.
- Tarehe 8 December ndio atapandishwa Mahakamani kusomewa mashitaka yake.
-
November 24 2014 Waziri wa mambo ya vijana wa Uganda aliitembelea
familia ya mtoto huyu baada ya watu kuanza kusambaza habari kwamba mtoto
huyu alifariki, taarifa ambazo sio za kweli.
إرسال تعليق