Mwanamke nchini Pakistan
Polisi
nchini Pakistan wanawashikilia wanaume watatu kwa kosa la utumizi dawa
za kulevya na ubakaji kwa mgonjwa aliyefuata matibabu katika hospitali
ya serikali.
Mwanamke huyo, ambaye alijifungua hivi
karibuni,alikwenda katika eneo la Burewala Mashariki ya jimbo la
Punjab,iliko hospitali hiyo na alikwenda hapo akiwa na mumewe pamoja na
mtoto wao mchanga kwa uchunguzi wa kitabibu.
Mume wa mwanamke huyo
alimwacha mkewe kitambo kifupi tu na aliporejea eneo alipokuwa
,hakumkuta ila mtoto na begi la mwanamke huyo vimetelekezwa.
Saa
kadhaa baadaye,alimpata mkewe akiwa amelala katika chumba chenye kiza
,kilichomo katika hospitali hiyo na kuthibitika kuwa amebakwa .
baada
ya fahamu kumrejea mwanamke huyo alisema kwanza alichomwa sindano na
wanaume hao watatu kisha wakaanza kumbaka kwa zamu.Wanaume wote hao ni
wanafanya hospitalini hapo.(BBC)
إرسال تعليق