
Meneja
wa Tigo kanda ya kusini, Bw.Daniel Mainoya (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu harambee inayojulikana kama Tigo Mtwara
Benefit Gala kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika wilaya ya Mtwara,
kushoto kwake ni mkuu wa wilaya hiyo,Bw. Wilman Ndile na kulia ni Meneja
maendeleo ya bishara kampuni ya 361 Degrees,Hamis Omary.
Tigo
Tanzania leo imetangaza kwamba itasaidia kujenga na kuchangia vifaa
katika maabara ya shule za sekondari ambazo zimekwisha jengwa wilayani
Mtwara. Mamlaka ya wilaya yanaandaa harambee kubwa siku ya Ijumaa wiki
hii kwa ajili kufanikisha jambo hili.
Akizungumza
wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo katika ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Mtwara, Meneja wa Kanda ya Mtwara kutoka Tigo Daniel Mainoya
alisema kwamba kampuni yake inaamini katika kuwapatia watoto mazingira
bora yakusomea, ili kuweza kuwajengea uwezo wa kuwa wananchi
wanaowajibika na kuzalisha ipasavyo.
“Hii
ni muhimu sana hasa hasa katika kujifunza masomo ya sayansi. Ni muhimu
kwa watoto wetu kupewa vifaa vinavyotakiwa ili kuweza kupata uelewa si
wa kinadharia tu bali wakiuzoefu wa namna ya kujifunza masomo ya sayansi
kama Baiolojia, Kemia na Fizikia,” alisema Mainoya.

Mkuu
wa wilaya ya Mtwara mjini Bw. Wilman Ndile (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu harambee inayojulikana kama Tigo Mtwara
Benefit Gala kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika wilaya ya Mtwara,
kulia kwake ni Meneja wa Tigo kanda ya kusini, Bw.Daniel Mainoya na
kushoto kwake mkurugenzi wa kampuni ya Proactive Solution, Nestory
Phoye.
Wilaya
ya Mtwara, ni moja kati ya wilaya sita zilizoko katika halmashauri ya
mkoa wa Mtwara, yenye jumla ya shule za sekondari 42 zinazoendeshwa
chini ya serikali. Kati ya hizi asilimia 18 tu ya shule hizi ndo zenye
maabara ya kujifunza Fizikia, Kemia na Baiolojia, kutokana na maelezo ya
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Kapenjama.
Akielezea
kwamba hali kuwa ni “mbaya,” Kapenjama aliwaambia waandishi wa habari
kwamba kukosekana kwa maabara hizo ni kilema kikubwa kwa wanafunzi
wanaoazimia kuja kufanya kazi katika tasnia ya sayansi kama madaktari,
maenjenia na kadhalika. Kutokana na maelezo ya DC alama ya wastani ya
ufaulu kwa wilaya ya Mtwara katika masomo ya sayansi kwenye shule za
sekondari kwa sasa ni asilimia 35.
“Ni
kwa sababu hii tuntoa rai kwa wadau wote kutoka katika sekta binafsi na
ya umma kuja kutuunga mkono katika kuchangisha fedha kujenga maabara
mapya na kuwapatia vifaa kwa maabara chache ambazo tayari zilishajengwa
ili kuweza kuwawezesha watoto wetu kufurahia masomo ya sayansi na wakati
huo huo kuweza kutimiza ndoto zao ya kuwa wanasayansi bora duniani,”
alisema
Harambee hiyo inayojulikana kama Tigo Mtwara Benefit Gala,
itafanyika Ijumaa hii na itajumuisha kampuni na watu binafsi, pia
kutakuwa kuna mnada wa bidhaa na vitu mbali mbali kama michoro ya
Kiafrika, Yakimakonde na mnada wa safari za kitalii nchini, yote haya ni
kwa ajili yakuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara 43 katika
sekondari mbali mbali hapa wilayani, alisema Kapenjama.
إرسال تعليق