Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Amesema ni vyema akabaki na kazi ya kupinga kwa ajili ya Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) badala ya kukitukana chama ambacho ndicho
kilichomuweka madarakani.
Nape alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara, mbele ya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana, katika muendelezo wa ziara yake
ya kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
mwaka 2010/2015.
"Maalim Seif aachie ngazi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ili afanye
kazi ya Ukawa ambayo haina lolote.Wameanza kutofautiana kwa ajili ya
uchaguzi wa Serikali za Mitaa,"alisema.
Alisema, Maalim Seif ambaye anazunguka na kuwaambia wananchi kuwa
CCM mbaya ni kuwahadaa Watanzania kwani kwa sasa maisha yake
yanaendeshwa na serikali ya chama hicho ambacho ndicho kinamlipa
mshahara.
Alisema, CCM haiko tayari kuacha wapinzani wakaenda Ikulu kwani
Ikulu kinakwenda chama cha siasa na siyo makundi ya wanaharakati.
"CCM inaweza kucheza na wapinzani katika maeneo mbalimbali lakini
si kwa kuwaacha washinde nafasi ya urais, ubunge na udiwani. Kifupi
upinzani hauwezi kwenda Ikulu," alisema Nape.
Alifafanua kuna tofauti kubwa kati ya CCM na wapinzani kwani CCM,
wanazungumzia maendeleo ya wananchi na wapinzani wanazungumza porojo na
kejeli na kutengeza chuki dhidi ya Watanzania.
CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق