MKALI
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, juzi
uusiku alikonga nyoyo za waalikwa na Wanachama wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), katika uzinduzi wa ‘CHADEMA Mtandao.’
Profesa Jay, ambaye alikuwa akisaidiana na msanii mwenzake Mbunge wa
Mbyea Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, walikuwa wakitambulisha nyimbo yao
inayokwenda kwa jina la M4C, ambayo wataiimbia katika ziara iliyopewa
jina la M4C Tour itakayoanza hivi karibuni.
Viongozi, wanachama na waalikwa wengine, walianza kushangilia mara tu
mshehereshaji wa uzinduzi wa CHADEMA Mtandao, Ester Wasira alipowataka
Profesa Jay na Sugu wapande jukwaani kutumbuiza kidogo na kuelezea namna
watakavyofanya ziara yao ya nchi nzima.
Kelele za kushangilia na kuonyesha vidole vitatu zilisikika wakati
wasanii hao wakichana mistari ya kuwataka Watanzania na wanachama wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutekeleza yale waliyokubaliana
katika muungano wao Oktoba 26 mwaka huu pale Jangwaji jijini Dar es
Salaam.
Mara baada ya kuimba wimbo mmoja, Sugu alisema kama ilifanikiwa
katika albam yake ya Antvirus, ndivyo atakavyohakikisha Albamu ya MC4
Tour inafanikiwa kwa kiwango kikubwa.
“Kama nilivyopiga katika ‘movement’ ya Antvirus nitakuwa balozi tena
kwenye ‘movement’ hii itakayokwenda nchi nzima kuhamasisha vijana
kujiandikisha kwenye ‘BVR’ pamoja na kuikataa katiba ya vijisenti … hii
ni zaidi ya tamasha la muziki ‘stay tuned’ inaanza ‘soon’ tu,” alisema
Sugu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Programu ya
CHADEMA Mtandao, imelenga kuwawezesha Watanzania kujiunga na chama hicho
kwa njia ya mtandao ili waweze kupata habari na kuchangia kwa ajili ya
mabadiliko.
Uzinduzi wa CHADEMA Mtandao, ulirushwa moja kwa moja na televisheni
ya ITV katika ukumbi wa Serena Inn jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa
na uwakilishi wote wa vyama vya siasa vinavyounda UKAWA ambavyo ni NLD,
CUF na NCCR-Mageuzi.
إرسال تعليق